Nenda kwa yaliyomo

Jorginho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jorginho akiwa Napoli.

Jorginho (alizaliwa Brazil, 20 Desemba 1991) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Italia ambaye anacheza kama kiungo wa timu ya Arsenal FC na timu ya taifa ya Italia.

Jorginho alihamia Italia akiwa na umri wa miaka 15, na kujiendeleza kwenye timu ya vijana wa Verona, kabla ya kukuzwa kwa timu kubwa. Wakati wa 2010-11, alipelekwa mkopo kwa Sambonifacese.

Mnamo Januari 2014, alihamia Napoli, ambako mara moja alishinda Coppa Italia na Supercoppa Italiana na mwaka 2018 alijiunga na Chelsea F.C. ambapo kwa miaka minne alifanikiwa kutwaa mataji ya Europa League, Champions League, UEFA Super Cup pamoja na kombe la dunia la FIFA kwa vilabu.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jorginho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.