Nenda kwa yaliyomo

John Sentamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Sentamu mbele ya kanisa lake wakati wa Pasaka 2007

John Tucker Mugabi Sentamu (* 10 Juni 1949 mjini Kampala, Uganda) ni askofu mkuu wa York na mkuu wa jimbo la kanisa Anglikana la York linalojumlisha daiyosisi za kaskazini ya Uingereza. Ana cheo cha heshima cha pili katika kanisa Anglikana la Uingereza baada ya Askofu Mkuu wa Canterbury.

John Sentamu ni askofu mkuu wa kwanza nchini asiye Mwingereza kiasili.

John Sentamu alizaliwa katika kijiji karibu na Kampala akiwa mtoto wa sita kati ya 13. Alisoma sheria kwenye Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala akawa mwanasheria kwenye mahakama kuu ya Uganda. Mwaka 1973 Idi Amin alimteua kuwa hakimu wa mahakama kuu. Lakini alimkasirisha diketa alipokataa kumwachisha huru binamu mmoja wa Amin. Akafungwa jela wiki tatu baada ya arusi yake kwa muda wa miezi mitatu. Baada ya kuuawa kwa rafiki yake askofu mkuu Janani Luwum aliamua kuondoka Uganda akaenda Uingereza.

Alianza kusoma theolojia kwenye Chuo Kikuu cha Cambridge akapokelewa kama padre wa Kanisa Anglikana mwaka 1979. Akapata cheo cha Ph. D. mwaka 1984. Baada ya kufanya kazi kama pdre msaidizi na padre kiongozi katika parokia kadhaa likuwa askofu msaidizi wa Stepney mwaka 1996; 2002 akawa askofu wa Birmingham. 2004 alikuwa risi wa harakati ya Youth For Christ na 2005 raisi wa YMCA. Mwaka huohuo alipewa cheo cha askofu mkuu wa York.

Sentamu alichukua uraia wa kiingereza na leo hii ni raia wa Uganda na Ufalme wa Maungano vilevile. Amemwoa Margaret Sentamu. Wana watoto wawili wakubwa Grace na Geoffrey pamoja na watoto wawili wa kulea.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]