John Gould Fletcher
John Gould Fletcher (3 Januari 1886 – 10 Mei 1950) alikuwa mwandishi na mhakiki wa uchoraji kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 1939 alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]John Gould Fletcher alizaliwa tarehe 3 Januari 1886 mjini Little Rock, Arkansas. Akasomea Chuo Kikuu cha Harvard miaka ya 1903 hadi 1907. Wakati mwingi wa maisha yake Fletcher aliishi Uingereza ambako akahusiana na washairi wengine kama Amy Lowell na Ezra Pound. Mwaka wa 1916 Fletcher alimwoa mke wake wa kwanza, Florence Emily “Daisy” Arbuthnot, akaishi nyumbani kwake hadi 1932 alipotengana naye akarudi Arkansas, Marekani. Mwaka wa 1936 alimwoa mke wake wa pili, Charlie May Simon. Fletcher alipatwa na unyogovu mara nyingi hadi kulazwa hospitalini, akajiua tarehe 10 Mei, 1950 nyumbani kwake mjini Little Rock.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Gould Fletcher kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |