John Bettis
John Bettis (amezaliwa tar. 24 Oktoba 1946) ni mshairi kutoka nchini Marekani. Huyu anafahamika sana kwa kushirikiana kwake kwenye utunzi wa nyimbo maarufu kwa miaka kadhaa. Awali alikuwa mmoja kati ya wanachama wa bendi ya Spectrum, ambaye pia ina wasanii wengine kama vile Richard na Karen Carpenter. Alitoa mashairi kadha wa kadha kwa ajili ya The Carpenters' ("Top of the World", "Only Yesterday", "Goodbye to Love"), na baadaye alitunga tena kwa ajili ya wasanii maarufu kama vile Madonna (""Crazy for You""), Michael Jackson ("Human Nature"), The Pointer Sisters ("Slow Hand") Diana Ross ("When You Tell Me That You Love Me"), Jennifer Warnes ("Nights Are Forever"), na Peabo Bryson ("Can You Stop the Rain"). Bettis pia alishiriki kwenye utunzi wa nyimbo ya "One Moment in Time", wimbo ulioimbwa kwenye 1988 Summer Olympics na Whitney Houston, na kibwagizo cha ucheshi wa miaka ile ya 1980 Growing Pains, "As Long As We Got Each Other."
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John Bettis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |