Mrifaki
Kundinyota | Farisi (Perseus) |
Mwangaza unaonekana | 1.82 |
Kundi la spektra | F5 I |
Paralaksi (mas) | 6.43 ± 0.17 |
Umbali (miakanuru) | 510 |
Mwangaza halisi | - –5.1 |
Masi M☉ | 8.5 ± |
Nusukipenyo R☉ | 68 ± |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 6,350 |
Majina mbadala | α Persei, 33 Persei, Marfak, Algenib, BD+49 917, CCDM J03243+4951A, FK5 120, GC 4041, HD 20902, HIP 15863, HR 1017, IDS 03171+4930 A, PPM 46127, SAO 38787 |
Mrifaki (lat. & ing. Mirfak pia α Alfa Persei, kifupi Alfa Per, α Per) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Farisi (Perseus) na nyota angavu ya 24 kwenye anga la usiku[2].
Jina
[hariri | hariri chanzo]Mrifaki inayomaanisha “kiwiko” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [3]. Walipokea jina hili kutoka Waarabu wanaosema المرفق al-mirfak inayomaanisha „kiwiko" [4]. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Mirfak" [5] .
Alfa Persei ni jina la Bayer kwa sababu Alfa ni herufi ya kwanza katika alfabeti ya Kigiriki na Mrifaki ni nyota angavu zaidi katika Farisi - Perseus.
Tabia
[hariri | hariri chanzo]Mrifaki iko kwa umbali wa miakanuru takriban 510 kutoka Jua letu na ni mfumo wa nyota mbili. Nyota kuu ni Mrifaki A iliyo na mwangaza unaoonekana wa 1.5 na mwangaza halisi ni -4.8. Spektra yake ni ya aina ya B2. Nyota ya pili B ina mwangaza unaonekana wa 7.5.
Miaka milioni 4.5 – 5 iliyopita Mrifaki ilikuwa nyota angavu kabisa kwenye anga la Dunia. Wakati ule umabli wake na Jua ulikuwa miakanuru 34 pekee na mwangaza wake ulioonekana ulikuwa -3.99.[6]
Kutokana na jotoridi kubwa kwenye uso wake sehemu kubwa ya mng’aro wake unatoka kwenye spektra ya urujuanimno (ultraviolet radiation) na Mrifaki ni chanzo kikubwa cha mnururisho huu angani[7].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ vipimo kufuatana na Lyubimkov, Leonid S.; et al. (February 2010)
- ↑ Perseus - Mirfak – α Persei tovuti ya constellation guide
- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ Waarabu walikuwa na jina mbadala الجانب al-janib au „upande“ na hili lilingia pia katia vitabu vya astronomia ya magharibi kama „Algenib“; ilhali hii ni pia jina la Gamma Persei haitumiwi tena sana kwa Perseus, ling. Allen (1899), uk. 331; Waswahili walikuwa pia na jina mbadala „Janabu Farisawi“ yaani „upande wa Farisi (Perseus)“
- ↑ Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
- ↑ Tomkin, Jocelyn (April 1998)
- ↑ Wilkinson, E.; Green, J. C.; McLean, R.; Welsh, B. (1996)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Constellation Guide:Perseus
- Perseus, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
- MIRFAK (Alfa Persei), kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
- Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Perseus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
- Lyubimkov, Leonid S.; et al. (February 2010), "Accurate fundamental parameters for A-, F- and G-type Supergiants in the solar neighbourhood", Monthly Notices of the Royal Astronomical Society, 402 (2): 1369–1379 online hapa