Jamilah Lemieux

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamilah Lemieux
Jamilah Lemieux kwenye Makumbusho ya Brooklyn mnamo 2015
Jamilah Lemieux kwenye Makumbusho ya Brooklyn mnamo 2015
Alizaliwa 22 July, 1984
Nchi Mmarekani
Kazi yake Mwandishi, mhariri, mkosoaji wa kitamaduni

Jamilah Lemieux (Amezaliwa 22 Julai, 1984) ni mwandishi, mwanasanaa na mhariri wa nchini Marekani.[1] Alipata umaarufu kwa blogu yake, The Beautiful Struggler. Ni mwandishi aliyekuwa akifanya kazi katika magazeti ya Ebony (magazine), Cassius Magazine, na Interactive One, pamoja na kituo cha redio cha Radio One, pia alikiuwa ni mtangazaji wa kipindi cha Mom & Dad Are Fighting.[2] [3]

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Lemieux alizaliwa na kukulia katika jiji la Chicago, Baba yake ni David Lemieux, mwanachama wa zamani wa chama cha Black Panther Party, aliYetokea katika filamu ya The Spook Who Sat by the Door mwaka 1973

Lemieux ana shahada kutoka chuo kikuu cha Howard.[4] na pia ni mwanachama wa Alpha Kappa Alpha.[1]

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Uandishi[hariri | hariri chanzo]

Mara baada ya kumaliza chuo kikuu, Jamilah alianza kazi ya uandishi, akiandika katika blog pamoja na mitandao ya kijamii, blog yake mara nyingi ilikuwa ikizungumzia masuala ya mahusiano.[5] Ni mshindi wa mara tatu wa tuzo za Black Weblog Awards.[onesha uthibitisho]

Mnamo Mwaka 2011, Lemieux alikuwa mhariri katika gazeti la Ebony Magazine. Mwaka 2014 alikuwa mhariri msaidizi na mwaka 2015 alikuwa mhariri mkuu

Makala za Lemieux zimekuwa zikitokea katika vyombo kadhaa vya habari kama Mic media company, Essence Magazine, The Nation, The Washington Post, The New York Times, na The Guardian, mara nyingi amekuwa akiandika pia kuhusiana na utamaduni.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Lemieux ana mtoto mmoja wa kike Naima (aliyezaliwa mwaka 2013).[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jamilah Lemieux kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.