James Prescott Joule

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
James Prescott Joule

James Prescott Joule (24 Desemba 181811 Oktoba 1889) alikuwa mwanafizikia kutoka nchini Uingereza aliyejipatia ridhiki za maisha yake kwa kuendesha kiwanda cha bia.

Alichangia mengi kuhusu elimu ya umeme na fizikia ya joto. Kuanzia 1840 alifanya majaribio alimotambua ya kwamba umeme ukipita kwenye kipitishio kama waya inakipashia joto. Baada ya majaribio mengine na vipimo vingi alitamka kanuni ya Joule: joto la kipitishio linalingana na zao la namba mraba ya mkondo wa umeme (ampea) na ukinzani wa umeme (omu)).

Kizio cha joto kilitwa baadaye "jouli" kwa heshima yake.

Pamoja na William Thomson aliendelea kuchunguza uhusiano kati ya gesi na joto. Wligundua ya kwamba gesi yenye nafasi ya kupanua inapoa yaani kupunguza joto. Alitmia ujuzi huu kwa kubadilisha gesi kuwa kiowevu na kutengeneza mashine za kupasha baridi.