Nenda kwa yaliyomo

Jali Nyama Suso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jali Nyama Suso (alizaliwa 1925 - 1991) alikuwa ni mpigaji wa kora nchini Gambia. Alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 1971 wakati akifundisha katika Chuo Kikuu cha Washington. Mnamo mwaka 1980 alifanya ziara nchini Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Uswidi. Suso alitunga kibwagizo cha filamu ya Roots. Mnamo mwaka 1960 alikua maarufu na kupata heshima kubwa kwa mpango wake wa kuimba wimbo wa taifa redioni. Mwaka 1991 alifariki kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu[1]

  1. "Nyama Suso, the late Gambian kora player". www.oberlin.edu. Iliwekwa mnamo 2018-04-18.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jali Nyama Suso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.