Nenda kwa yaliyomo

J. C. Hayward

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
J. C. Hayward
Hayward akizungumza katika Taasisi za Kitaifa za Afya na Taasisi ya Historia ya Afrika na Amerika mwaka 2012
Hayward akizungumza katika Taasisi za Kitaifa za Afya na Taasisi ya Historia ya Afrika na Amerika mwaka 2012
Nchi Marekani
Kazi yake Mwandishi wa habari
kushoto kwenda kulia, Hayward, pamoja na Francis Collins, Griffin Rodgers, Janine Austin Clayton kwenye Maadhimisho ya Mwezi wa Historia ya NIH Amerika yenye asili ya Kiafrika mnamo mwaka 2012

J. C. Hayward (alizaliwa 23 Oktoba 1945, anajulikana pia kama Jacqueline Hayward Wilson) ni Mmarekani ambaye ni Msoma habari. Alifanya kazi na televisheni ya WUSA9 huko Washington, DC.Anajulikana sana kwa kuwa mtangazaji wa kwanza wa habari wa kike huko Washington, DC na mtangazaji wa kwanza wa habari wa kike wa Kiafrika wa Amerika. Katika nyakati za hivi karibuni, Hayward alihusika katika Kashfa ya Mkataba na kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti.[1]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Jacqueline Hayward Wilson, anayejulikana zaidi kama J. C. Hayward, alizaliwa mnamo Oktoba 23 mwaka 1945 huko East Orange, New Jersey.[2] Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Howard akiwa na digrii za pamoja ya lugha ya Kiingereza na lugha ya Kihispania.[3] Amepokea pia shahada mbili za heshima za udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Howard na Chuo Kikuu cha Southeastern University.[4] Mwaka 1972, Hayward alianza kufanya kazi katika chombo cha habari cha WUSA9 kama msomaji wa habari na akakaa hapo hadi kustaafu kwake mwaka 2015.

Mwaka 2012, Hayward aligunduliwa kuwa na hatua ya pili ya saratani ya matiti.[5][1] wiki moja tu baada ya uchunguzi kufanyika, uvimbe uliondolewa na kutangazwa kuwa hana saratani.[5] Mwaka 2013, J. C. Hayward alitajwa katika mashtaka na Shule ya Public Charter School.[6]lakini baadaye mwaka huo huo aliondolewa kutoka kwenye kesi hiyo na kuachiliwa kutokana na madai hayo.[7]J. C. Hayward kwa sasa anakaa "Fort Lauderdale, Florida", kwa miaka mingi.[8]

Kazi na WUSA9

[hariri | hariri chanzo]

J. C. Hayward alianza kufanya kazi katika chombo cha habari cha WUSA9 kama msomaji wa habari mwaka 1973. Wakati alipokuwa akifanya kazi ya habari WUSA9, Hayward alipewa sifa ya kuwa msoma habari wa kwanza wa kike huko Washington, D.C.[1] alipokuwa anafanya kazi, watu walikuwa wakizungumzia sana Hayward, walisema alijua wakati wa kufanya kazi lakini pia alijua wakati wa kufurahi. Hayward alihusika sana na jamii ambayo ilimsababisha jamii kumuona alikuwa mwaminifu na kituo cha habari.[3] Along with anchoring on WUSA9 News Now at Noon, Hayward also produced 'JC and Friends'[9] J. C. Hayward pia alikuwa [[Makamu wa rais wa media outreach for the station.

Mnamo 2013 Hayward alisimamishwa kazi hewani baada ya kutajwa katika mashtaka ya shule ya Charter school.[6]Alipewa likizo kwenye kituo alichokuwa akifanyia kazi wakati wa uchunguzi zaidi.[10] Muda mfupi baadaye,mwaka 2015, baada ya karibu miaka 43 ya kufanya kazi katika chombo cha habari cha WUSA9, J. C. Hayward alitangaza kustaafu kufuatia madai hayo.[1]

Kazi mashuhuri za uandishi wa habari

[hariri | hariri chanzo]

J. C. Hayward amepata heshima ya kufanya kazi na wageni wengi mashuhuri wakati wote wa kazi yake. Katika maisha yake, Hayward alipata nafasi ya kufanya mahojiano na watu mashuhuri wakiwemo, "Maya Angelou", "Luciano Pavarotti", na Mke wa Rais "Nancy Reagan".[4][11]Pamoja na mahojiano hayo, Hayward pia alisimamia hafla kubwa wakati wa enzi yake, kwa mfano J. C. aliweza kusimamia ugeni wa Rais wa Afrika Kusini "Nelson Mandela" alipotembelea Merekani. Wakati Mandela alipokuwa ziarani, pia alipata nafasi ya kufanya mahojiano ya kipekee naye. Hayward pia alikuwa mfanya mahojihano kwa "Kila Wanawake," kipindi cha mazungumzo ya kila siku kwenye Channel 9.[4] kipindi cha mwezi wa watu wenye asili ya Kiafrika nchini Marekani, Alifanya kipindi cha Nine who care kwa watu walio kuwa wanajitolea kwenye jamii.[3]

Alikuwa akihusika katika mashirika yanayo jihusisha na miradi ya jamii, kwa mfano alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini kwenye shule ya Public Charter School. Alikuwa pia mjumbe wa bodi ya Kituo cha Perry Center, Huduma ya Hospitali, Huduma za Dini mbili, Mfuko wa Ulinzi wa Sheria wa NAACP, Summer Opera Theatre Company, na United Black Fund.[4] Hayward alisaidia vilabu vya wavulana & wasichana nchini Marekani ya Greater Washington.[3] In 2012, she also served as the Gala Chair for Arena Stage.[4]

Baada ya kupigana afya kutokana na saratani ya matiti, Hayward aliwahimiza wanawake wamakimarekani wenye asili ya kiafrika kupata chanjo ya mammograms.[12]

Katika kipindi chote cha kazi yake ya uhandishi wa habari, J. C. Hayward alipokea tuzo nyingi na sifa kwa kazi yake. Mwaka wa 1972, Hayward alipokea local Emmy's kwaajili ya makala yake "" Sahel: The Border of Hell"." Mwaka 1976, Hayward alitunukiwa tuzo nyingine ya local Emmy kama Best mtangazaji wa habari. Mwaka 1980, alipata Nishani ya Shaba kutoka International Film Festival kutokana na makala ya'We Shall Return'. Baada ya kuhojiana na bondia Riddick Bowe, Hayward alipokea local Emmy nyingine mwaka 1994. Mwaka 1995, aliteuliwa na kupokea Tuzo ya Bodi ya Gavana pamoja na kupata tuzo nyingine ya local Emmy "Licha ya mafanikio yake hayo ya kipekee yaliyo onyehsa uimara wake katika habari." = arthritismar /> Mwaka wa 2000, Hayward aliingizwa kwenye kwenye historia ya waandishi wa Habari maarufu na Jamii ya Wanahabari Wataalamu.[11] In 2007, Hayward was awarded her final local Emmy in the category of Outstanding Community Affairs. Along with all of the local Emmy, Hayward amewahi kuwa miongoni mwa waliopewa tuzo ya "Washingtonian of the Year." mwaka 2011, J. C. Hayward aliwahi pia kupata tuzo ya kitaifa ya The National Association of Black Journalists Hall of Fame.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "JC Hayward Retiring from WUSA". www.adweek.com.
  2. "Happy Birthday JC Hayward! | Afro", Afro, October 24, 2012. Retrieved on January 10, 2018. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Roberts, Roxanne (Februari 21, 2002). "J.C. Hayward, Anchor Of the Community" – kutoka www.washingtonpost.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 https://arthritismar.ejoinme.org/MyEvents/2013DCPurseswithPower/AbouttheHostess/tabid/445545/Default.aspx
  5. 5.0 5.1 "JC Hayward and Andrea Roane: "Buddies" through Breast Cancer - Prevent Cancer Foundation–Stop Cancer Before It Starts!". preventcancer.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-10. Iliwekwa mnamo 2021-05-22.
  6. 6.0 6.1 "WUSA Anchor Named in Lawsuit and 'Relieved of Her Duties'". www.adweek.com.
  7. Chandler, Michael Alison (Agosti 11, 2015). "Ex-anchor J.C. Hayward dismissed from Options charter lawsuit" – kutoka www.washingtonpost.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Chandler, Michael Alison; Brown, Emma (Januari 23, 2015). "J.C. Hayward announced retirement from WUSA9 following long hiatus amid charter school investigation" – kutoka www.washingtonpost.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "A No C's Weekend in Washington, D.C. « Face of America". www.faceofamericawps.com.
  10. Brown, Emma (Desemba 17, 2013). "J.C. Hayward: A long-time local benefactor awaits a legal resolution" – kutoka www.washingtonpost.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. 11.0 11.1 Halper, Donna (Februari 11, 2015). Invisible Stars: A Social History of Women in American Broadcasting. Routledge. ISBN 9781317520177 – kutoka Google Books.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "J.C. Hayward discusses breast cancer diagnosis". Washington Post. Aprili 10, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu J. C. Hayward kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.