Nenda kwa yaliyomo

Ismaël Bennacer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ismaël Bennacer

Ismaël Bennacer (alizaliwa tarehe 1 Desemba 1997) ni mchezaji wa soka wa kulipwa anayecheza kama kiungo wa kati katika klabu ya AC Milan. Akiwa amezaliwa Ufaransa, anawakilisha timu ya taifa ya Algeria.

Katika ngazi ya vilabu, Bennacer amechezea timu nchini Ufaransa, Uingereza na Italia katika kipindi chake cha kazi. Katika ngazi ya kimataifa, alicheza kwanza mechi yake ya kimataifa kwa Algeria mwaka 2016, na tangu hapo ameiwakilisha nchi yake katika matoleo matatu ya Kombe la Mataifa ya Afrika; alikuwa mwanachama wa timu iliyoshinda toleo la 2019, na aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Kazi ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Ingawa hapo awali aliwahi kuiwakilisha Ufaransa katika ngazi ya vijana, tarehe 31 Julai 2016, Shirikisho la Soka la Algeria lilitangaza kuwa Bennacer alikuwa ameamua kubadilisha uraia wake wa kimichezo na kuiwakilisha Algeria kimataifa.[1] Alicheza mechi yake ya kwanza na Algeria katika Mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017, ambapo Algeria ilishinda dhidi ya Lesotho mabao 6–0.[2]

Mnamo tarehe 11 Januari 2017, Bennacer aliitwa kwenye kikosi cha Algeria kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika cha mwaka 2017[3] kuchukua nafasi ya Saphir Taïder, ambaye alipata jeraha wakati wa mazoezi.[4]

Katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2019, Bennacer alisaidia Algeria kutwaa taji lao la kwanza baada ya miaka 29, akimaliza mashindano hayo akiwa mtoa pasi bora zaidi kwa pamoja na Franck Kessié, kila mmoja akiwa na pasi tatu za mabao, ikiwemo moja iliyomsaidia Baghdad Bounedjah kufunga bao la ushindi dhidi ya Senegal katika fainali ya michuano hio ya tarehe 19 Julai.[5][6][7] Baadaye alichaguliwa kuwa "Mchezaji Bora Chipukizi" na pia "Mchezaji Bora wa Mashindano hayo".

Mwezi Desemba 2023, aliitwa kwenye kikosi cha Algeria kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023.[8]

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

Empoli

  • Serie B: 2017–18

AC Milan

  • Serie A: 2021–22[9]

Algeria

Binafsi

  • Mchezaji Bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika: 2019
  • Timu ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya CAF: 2019[11]
  1. Toufik O. (31 Julai 2016). "Bennacer (Arsenal) choisit officiellement l'Algérie" (kwa Kifaransa). DZfoot. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "CAN 2017 : Algérie 6-0 Lesotho" (kwa Kifaransa). DZfoot. 4 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Arsenal midfielder Ismael Bennacer handed shock call up to Algeria's Africa Cup of Nations squad". Metro.co.uk. 11 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. M-A-D (11 Januari 2017). "CAN 2017 : Ismael Bennacer remplace Taider" (kwa Kifaransa). DZfoot. Iliwekwa mnamo 11 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Algeria celebrate second Afcon title after beating Senegal". BBC Sport. 19 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "AC Milan snap up Algeria's Africa Cup star Bennacer". The Score. 4 Agosti 2019. Iliwekwa mnamo 4 Agosti 2019.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Otieno, Imran (20 Julai 2019). "Top Assists charts at the 2019 African Cup of Nations". futaa.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Mei 2022. Iliwekwa mnamo 4 Agosti 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "CAN 2024 : L'Algérie Dévoile sa Liste Officielle – Qui Sont les Fennecs Prêts à Conquérir l'Afrique ?" (kwa Kifaransa). Algérie-Focus. 30 Desemba 2023. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Milan secure 1st Serie A title in 11 years". News18 India. 22 Mei 2022. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Algeria hold on against Senegal to win Afcon". BBC Sport. 19 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Kappel, David (21 Julai 2019). "Caf Announces Afcon Team of The Tournament". www.soccerladuma.co.za. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 25 Julai 2019. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ismaël Bennacer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.