Isha Ramadhani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Isha Ramadhani
Isha Ramadhani akitumbuiza
Isha Ramadhani akitumbuiza
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Isha Ramadhani
Pia anajulikana kama Isha Mashauzi
Mamaa wa Mashauzi
Mamaa Ina-Hu
Amezaliwa 3 Februari 1982 (1982-02-03) (umri 42)
Asili yake Mwanza
Tanzania
Aina ya muziki Taarab
Miaka ya kazi 2006-hadi leo
Ame/Wameshirikiana na Mzee Yusuf
MC Babu Ayubu

Isha Ramadhani (amezaliwa 3 Februari 1982) ni mwimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo za taarab kutoka nchini Tanzania.

Anafahamika sana kwa kuwa mmoja kati ya walioanzisha kundi zima la taarab la Jahazi Modern Taarab. Kundi ambalo linaongozwa na Mzee Yusuf. Bi. Isha alizaliwa mkoani Mwanza, akiwa mtoto wa kwanza kati ya watoto watano katika familia yake. Alisoma shule ya msingi Mnazi Mmoja huko jijini Dar es Salaam kuanzia mwaka wa 1990 hadi 1996 alipomaliza darasa la saba.

Kwa bahari nzuri, kabahatika kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini aliishia kidato cha pili shuleni hapo kwa kutokana na matatizo mbalimbali ya kifamilia. Isha, ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Mara, hivi sasa ameolewa na ana watoto wawili. Anaishi na familia yake maeneo ya Tandale, Dar es Salaam.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Mara yake ya kwanza kupanda jukwaani na kuimba na kundi la Jahazi, ilikuwa kwenye onyesho lililofanyika kwenye ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi, Oysterbay, Dar es Salaam. Katika onyesho hilo, aliimba wimbo wa "Hayanifiki" ambao umempatia umaarufu kwa kiasi kikubwa na kumfanya atambulike kwenye ulimwengu wa muziki wa taarab nchini Tanzania. Tangu hapo, akawa anashiriki kwenye vibao kadha wa kadha. Kibao hicho kilitungwa na Mzee Yusuf.

Miaka miwili baadaye, alifanikiwa kutunga wimbo wake mwenyewe, unaotambulika kwa jina la "Ya Wenzenu Midomo Juu". Wimbo ambao unapatikana kwenye albamu ya "VIP", ambayo ni ya nne kwa Jahazi. Wimbo huo ulimfanya awe juu na kuweza kupata mashabiki wengi zaidi kwenye ulimwengu wa mipasho.[1]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isha Ramadhani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.