Nenda kwa yaliyomo

Askari wa miguu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Infantry)

Askari wa miguu (kwa Kiing. infantry) ilikuwa tawi la jeshi la nchi katika mpangilio uliotofautisha askari wa miguu, askari farasi na matawi maalum kama askari wa mizinga na mapayonia. [1]

Katika majeshi ya kisasa askari farasi hawako tena na karibu askari wote hutumia vyombo vya usafiri.

Hata hivyo, jina la askari wa miguu (infantry) bado hutumiwa kutaja askari ambao wanapiga vita moja kwa moja wakitumia vyombo kwa usafiri, si kama zana za mapigano.

Hao askari wa miguu kwa kawaida huathiriwa zaidi katika mapigano kulingana na matawi mengine ya jeshi, maana ni hao wanaojeruhiwa na kuuawa zaidi.[2] Hivyo hutazamwa kuwa sehemu muhimu ya jeshi la ardhi.

Kihistoria, askari wa miguu walitumia mikuki, panga, pinde na ngao. Askari wa miguu wa kisasa wanajifunza kutumia aina nyingi tofauti za silaha, zikiwemo bunduki, mabomu ya mkononi, virusha roketi, bastola na bombomu .

  1. "infantry". Dictionary.com. Iliwekwa mnamo 12 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. In Praise of Infantry, by Field Marshal Archibald Wavell, 1st Earl Wavell, The Times, Thursday, 19 April 1945