Ikram Kabbaj

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ikram Kabbaj (kwa Kiarabu: إكرام القباج; alizaliwa mwaka 1960) ni msanii anayejishughulisha na sanaa ya uchongaji kutoka Morocco. Kabbaj kwa kiasi kikubwa huchonga vitu kutoka kwenye mawe na marumaru.

Maisha Ya Awali Na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kabbaj Alizaliwa Casablanca mwaka wa 1960. Alipata elimu yake kutoka shule ya sanaa École des Beaux-Arts huko Paris, akisoma huko kutoka mwaka 1978 hadi 1987 akibobea katika sanaa ya uchongaji.

Kazi Na Sanaa[hariri | hariri chanzo]

Kazi na sanaa za Kabbaj huoneshwa kwa kiwango cha kitaifa nchini Morocco na kimataifa.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Ikram Kabbaj". Beauce Art (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2019-10-26.