Nenda kwa yaliyomo

Ikozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ikozi ni kata ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini katika Mkoa wa Rukwa, Tanzania.

Kata inaundwa na vijiji vya Ikozi, Chituo, Kazwila, Tentula na Lula. Ukiachana na Laela (mji mdogo), Mpui, na Kaengesa, Ikozi inafuata kwa ukubwa katika vijiji vilivyopo kwenye barabara kuu ya Tunduma-Sumbawanga vilivyopo mkoa wa Rukwa.

Kijiji cha Ikozi kina shule tatu za msingi, mbili za umma (Ikozi na Kazwila) na moja ya binafsi huku ikiwa na sekondari mbili, moja ya mtu binafsi (Fingwa) na nyingine ya umma (ujenzi haujakamilika).

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,500 [1].

Kata za Wilaya ya Sumbawanga VijijiniMkoa wa Rukwa - Tanzania

Ikozi | Ilemba | Kaengesa | Kalambanzite | Kalumbaleza | Kanda | Kaoze | Kapenta | Kasanzama | Kilangawana | Kipeta | Laela | Lusaka | Lyangalile | Mfinga | Miangalua | Milepa | Mnokola | Mpui | Mpwapwa | Msandamuungano | Mtowisa | Muze | Mwadui | Nankanga | Sandulula | Zimba


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ikozi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.