Iker Casillas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Iker Casillas

Iker Casillas Fernández(alizaliwa 20 Mei 1981) ni mchezaji kutoka Hispania anayecheza kwenye klabu ya FC Porto na timu ya taifa ya Hispania kama golikipa. Cassilas anajulikana kama golikipa mwenye mafanikio makubwa kwa muda wote katika soka.Casillas alianza kucheza mpira mwaka 1999 katika timu ya wadogo ya Real Madrid. Akiwa Madrid Casillas alipata mafanikio mengi ikiwemo kuchukua kombe la UEFA mara tatu na kuchukua kombe la LA LIGA. Katika timu ya taifa Casillas amefanikiwa kuiwezesha kuchukua kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini walipocheza fainali na timu ya taifa ya Uholanzi. Kwenye mafanikio yake amewahi kushinda tuzo ya golikipa bora wa dunia nyuma yake akiwa Buffon wa Italia mwaka 2010.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Iker Casillas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.