IHH

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

İHH İnsan Yardım Vakfı (jina kamili Kituruki: İnsan Hak ve Hürriyetleri ve İnsani Yardım Vakfı, kwa Kiswahili: Shirika la Haki za Binadamu, Uhuru na Msaada) ama IHH kwa kifupi ni shirika la kituruki la kibinafsi linalotoa msaada katika nchi zaidi ya 100.[1] Shirika hili lilianzishwa katika mwaka wa 1992 na kusajiliwa rasmi Istanbul mwaka wa 1995.IHH inatoa msaada katika sehemu zilizokumbwa na vita, njaa na mtetemeko wa ardhi ama majanga mengine ya asili.

IHH ilikuja katika tahadhari la kimataifa baada ya meli zake za kimsaada zilizokuwa zinapeleka msaada Gaza kushambuliwa na makomando toka Israeli.Wafanya kazi tisa wa IHH katika meli MV Mavi Marmara waliaga dunia na wengine wengi kujeruhiwa.

Hakimu Jean-Louis Bruguière wa shirikisho la kifaransa la kupambana na magaidi, mshauri wa kimataifa katika mambo ya kigaidi Evan Kohlmann, pamoja na serikali ya Israeli ina madai kuwa IHH ina uhusiano na Hamas na makundi mengine ambayo serikali kadhaa zimehusisha na ugaidi. IHH imepinga madai hayo.

Uanzishi[hariri | hariri chanzo]

Shirika la kibinafsi la Misingi ya haki za kibinadamu, Uhuru na Msaada (IHH) lenye makao yake makuu mjini Istanbul ni shirika binafsi la kiislamu ambalo lilianzishwa ili kutoa msaada kwa waislamu nchini Bosnia katika miaka ya 90. Imetoa msaada katika nchi kama Pakistan, Ethiopia, Lebanon, Indonesia, Iraq, Palestina, Sudan, Ghana, Mongolia, China, Brazil, Argentina na sehemu zingine nyingi. Imepigwa marufuku nchini Israeli kwa kutoa msaada kwa Hamas.

Ingawa linakubalika kama kundi la kiislamu, shirika hili linatoa msaada kwa watu wote wanaohitaji msaada bila pingamizi la kidini. IHH imekuwa ikitoa ushauri maalum katika baraza la Muungano wa Mataifa ya Uchumi na Jamii tangu 2004. IHH ni msimamizi mkuu wa mpango kupambana na magonjwa ya macho barani Afrika.

Shughuli za kibinadamu[hariri | hariri chanzo]

IHH inahusika katika shughuli za kijamii na kitamaduni, pamoja na huduma za afya katika nchi zaidi ya 100.Linasimamia msingi wa kupambana na magonjwa ya macho barani Afrika lililoanza mwaka 2007 katika nchi kumi. IHH ilituma toni 33 za msaada Haiti baada ya nchi hiyo kukumbwa na mtetemeko wa ardhi mwaka 2010.

Mwaka wa 2007 mwezi wa desemba gazeti la Today's Zaman liliandika kwamba "mashirika ya kirai mbalimbali kama Kimse Yok Mu?, Deniz Feneri, Can Suyu na IHH ziliwezesha watoa misaada wengi kufikisha kufikisha misaada yao katika eneo la kikurdi linalokumbwa na umaskini mashariki na kusini mashariki mwa uturuki ".[2]

Gazeti la World Bulletin la Agosti 2009 liliandika kwamba mamia ya visima na chemichemi zilitengenezwa katika juhudi za kimsaada zilizopangwa na IHH. Pia ilikuwa moja ya mashirikisho mengi ya kibinadamu yaliyotoa msaada Bangladesh baada ya mafuriko kukumba nchi hiyo.

IHH katika miaka ya mwanzo ilituma misaada ya unga, mafuta na sukari kwa familia 350 zinazoishi Zewaya Dugda nchini Ethiopia ambayo ni sehemu inayokumbwa na umaskini.

Flotilla la Gaza[hariri | hariri chanzo]

Januari 2010 IHH pamoja na kundi la harakati za Uhuru wa Gaza zilitangaza kuwa zitatuma meli za misaada kuelekea Gaza mwezi wa tano, mpango huu ulialika miungano mingine kutoka Ugiriki, Ireland na Sweden. 30 Mei 2010, kundi la meli sita zilizobeba wanaharakati 663 kutoka mataifa 37 zilianza safari ya kuelekea Gaza. Lengo kuu la safari hii ilikuwa kuvunja umarufuku uliowekwa na nchi ya Israeli kuzuia misaada yoyote kuingia Gaza.

31 Mei 2010, Makomando wa Israeli walivamia meli hizo zilipokuwa katika maji ya kimataifa. Katika mapambano hayo wanaharakati 9 katika meli ya MV Mavi Marmara walipigwa risasi na kuuliwa na wengine wengi walijeruhiwa kati yao makomando saba wa Israeli. Makomando waliiteka meli hiyo na kuipeleka katika bandari la Ashdod nchini Israel. Misaada ilishushwa na kukaguliwa kabla ya kupelekwa Gaza. Hamas walikataa misaada hiyo hadi wanaharakati wote waliokuwa wameshikwa waachiliwe. Mashambulizi haya yalikasirisha mataifa mengi na kufanya Serikali ya Misri kufungua mpaka wake na Gaza wa Rafah.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Profile: Free Gaza Movement", BBC News, BBC, 2010-06-01. Retrieved on 2010-06-05. 
  2. "Sherehe za Iddi za leta umoja Uturuki". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-23. Iliwekwa mnamo 2010-07-08. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]