MV Mavi Marmara
MV Mavi Marmara (kwa Kiswahili: Buluu Marmara) ni meli ya kubeba abiria ya kisiwa cha Komori inayomilikwa na shirika la İDO Istanbul Fast Ferries Co. Inc. katika bahari ya Marmara.
Msafara wa meli wa Gaza
[hariri | hariri chanzo]Meli hii ilinunuliwa na shirika la msingi za Haki za kibinadamu, Uhuru na Msaada IHH mwaka 2010.Shirikisho hili linahusika katika harakati za kutoa misaada katika nchi zaidi ya 100. Meli hii iliungana na meli zingine katika msafara huu ambao lengo lake maalum ilikuwa kuvunja pingamizi la nchi ya Israeli kuzuia misaada kuingia Gaza. Kwa kuwa hamna shirika lililotaka kutia meli zake katika hatari IHH ililzimika kununua meli hiyo kwa bei $800,000 ambayo ilipatikana kutoka kwa michango.
Tarehe 31 Mei 2010, wakati meli hiyo ilipokuwa ikielekea Gaza, ilivamiwa na makomando wa israeli kisha wakaipeleka kwenye bandari ya Ashdod nchini Israel. Katika mapambano hayo wanaharakati 9 walikufa na wengine wengi kujeruhiwa.