Huntley & Palmers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mojawapo ya picha za kutangaza na kusifia biskuti za Huntley & Palmers
Mojawapo ya picha za kutangaza na kusifia biskuti za Huntley & Palmers
Mojawapo ya mikebe ya biskuti za Huntley & Palmers ikihifadhi biskuti za aina ya Marie
Mojawapo ya mikebe ya biskuti za Huntley & Palmers ikihifadhi biskuti za aina ya Marie

Huntley & Palmers ilikuwa kampuni ya Uingereza ya kupika biskuti waliokuwa na makao yao Reading,Berkshire. Kampuni hii iliunda mojawapo ya bidhaa za kimataifa za kwanza duniani na iliwahi kuwa kampuni kubwa kabisa ya utayarishaji wa biskuti duniani. Katika miaka ilyopita, kampuni ilijulikana kama J.Huntley & Son na Huntley & Palmer. Biashara ya utayarishaji wa biskuti ya jina lilo lilianzishwa hivi majuzi Sudbury,Suffolk. Tangu mwaka wa 1985, kampuni ya New Zealand,Griffin's Foods, ilianza kutayarisha biskuti za Huntley na Palmers chini ya leseni kutoka kampuni mzazi. [1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Joseph Huntley[hariri | hariri chanzo]

Huntley & Palmers ilianzishwa katika mwaka wa 1822 na Joseph Huntley akaiita J. Huntley & Son. Hapo awali,biashara yao ilikuwa kutayarisha biskuti na switi tu katika duka la nambari 72,barabara ya London. Wakati huo,barabara ya London ndiyo iliyokuwa kituo cha kusimama kwa wasafiri wakielekea Bristol,Bath na West Country. Mojawapo ya vituo vya kuita wasafiri kuingia kwenye mbinu zao za usafiri,ilikuwa Crown Inn,iliyokuwa karibu na duka la Joseph Huntley na akaanza kuuza biskuti zake kwa wasafiri. Kwa sababu biskuti zillikuwa dhaifu na kuweza kuvunjika katika safari,alianza kuziweka ndani ya mkebe wa chuma. Ubunifu huu ulikuza biashara mbili: duka la biskuti za Joseph lililokuja kujulikna kama Huntley & Palmers, na Huntley,Bourne & Stevens-kampuni ya kuunda mikebe ya chuma iliyoanzishwa na mwana wa Joseph aliyeitwa,pia, Joseph.

George Palmer[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 183, Joseph Huntley alilazimishwa na shida za kiafya kustaafu ,akampa mwana wake mkubwa kabisa ,Thomas, biashara hiyo. Mwaka wa 1841, Thomas alimchukua kama George Palmer kama mshiriki katika biashara ,binamu wake na mwanachama wa Society of Friends. George Palmer alikuwa mkuu wa kuendesha mafanikio katika kampuni hiyo huku akianzisha vituo vya kuuza kote nchini. Kampuni ikawa kubwa kuliko duka lake la awali haraka sana na ikahamishwa hadi kiwanda kilichokuwa kwenye barabara ya King's Road karibu na reli la Great Western.Huu ulikuwa mwaka wa 1846. Kiwanda kilikuwa na mfumo wake wa reli ya ndani na magari yake ya mvuke yenyewe na mmoja ya haya limewekwa katika Jumba la Kumbukumbu. Hivi sasa ,limehifadhiwa mjini Kent [3]

Thomas Huntley alikufa katika mwaka wa 1857, lakini George Palmer aliendelea kuongoza kampuni kwa mafanikio huku akisaidiwa na ndugu zake William Isaac Palmer na Samuel Palmer na ,baadaye, wana wake wlichukua usukani wa kampuni. Walikuwa watayarshaji wa biskuti wa familia ya mfalme ya Uingereza na katika mwaka wa 1865 wakaendelea na upanuzi wao ndani ya bara la Uropa. Wakapata vibali vya kutayarishia familia ya ufalme nkutoka kwa Napoleon III na Leopold III wa Ubelgiji. Walipokuwa wamefanikiwa sana, walikuwa wameajiri watu 5,000 na katika mwaka wa 1900 walikuwa kampuni kubwa kabisa ya kutayarisha biskuti duniani. Mwanzo wa mafanikio ya kampuni ilitokana na sekta kadhaa. Walianzisha bidhaa mbalimbali maarufu, wakitayarisha bidhaa 400 tofauti illipokuwa ikifika mwaka wa 1903.Uzalishaji wa wingi uliwawezesha kuweka bei nzuri kwa bidhaa zao.

Palmers walikuwa watu mashuhuri sana katika eneo la Reading waliotoa hela nyingi na ardhi kwa ukarimu:Palmer Park ikiwa moja yao na mji huo ukajulikana kwa jina la utani la "mji wa biskuti".

Biashara za ng'ambo[hariri | hariri chanzo]

Sehemu nyingine muhimu iliyosababisha ufanisi katika kampuni ilikuwa uwezo wao wa kusafirsha biskuti zao ulimwengu nzima,zikiwa zimehifadhiwa vizuri, katika mikebe mizuri iliyopodolewa. Mikebe hii ilikuwa chombo muhimu katika uuzaji wa bidhaa zao ikiwa chini ya picha iliyojulikana sana ya Huntley & Palmer. Mikebe hii ilikuja kuashiria mfano wa nguvu wa jina ama chombo katika biashara kama kampuni ya Coca Cola,Marekani. Mikebe hii ilipata njia ya kufika ng'ambo hadi bara la Afrika na milima ya Tibet,kampuni hii ilimpa biskuti Nahodha Scott katika safari yake ya kuenda Ncha ya Kusini. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walizalisha biskuti za vita na wakatumia vifaa vyao vya kuunda mikebe ili kuunda zana za vita.

Muungano na baada ya muungano[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 1921, Huntley & Palmers walijiunga na kampuni pinzani ya Peak Frean, ikasababisha kuundwa kwa kampuni ya Associated Biscuit Manufacturers.Hata hivyo, kampuni hizo mbili zilihifadhi majina yao na maeneo yao ya kazi.

Mnamo mwaka wa 1960, Jacob's iliungana na kampuni hiyo ya ABM na ilipofika 1969,ilijulikana tu kama Associated Biscuits

Utayarishaji katika eneo la Reading uliachishwa katika mwaka wa 1976. Mwaka 1982, Nabisco ilinunua AB. Uzalishaji uliendelea huko Huyton hadi 1983. Baada ya kufungwa kwa kiwanda cha Peak Frean katika eneo la Bermondsey (1989),Nabisco iliuzia Danone bidhaa za AB(Huntley & Palmers,Peek Frean na Jacob's).

Kampuni hii iliunda bidhaa za aina 400 tofauti kwa miaka mingi na ikabuni biskuti za aina mingi sana:ile maarufu ya Nice ikiwa moja yao.

Wakati uliopita[hariri | hariri chanzo]

Historia ya kampuni ipo katika kitabu, Quaker Enterprise in Biscuit: Huntley and Palmers of Reading, 1822-1972 kilichoandikwa na Tab Corley, kilichochapishwa katika mwaka wa 1972 ili kukumbuka miaka 150 ya kampuni hiyo. Historia ya kampuni ipo katika Jumba la Kumbukumbu la Reading, lililo na maonyesho ya picha ya kampuni hii.

Kuanzishwa tena[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 2006, Huntley & Palmers ilianza opersheni zake tena Sudbury,Suffolk. Usimamizi mpya inahusu mtu aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa masoko na mauzo wa Jacob's Bakery na mwanzilishi wa Vibrandt,kampuni maarufu ya kuunda pakiti. Wanalenga sekta ya vyakula vitamu na spesheli.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Huntley & Palmers Archived 17 Februari 2023 at the Wayback Machine.
  2. Maelezo ya ziada
  3. Kuhusu historia ya kampuni.Huntley and Palmers Archived 17 Januari 2010 at the Wayback Machine.
  4. Wakati wa Biskuti Archived 7 Oktoba 2011 at the Wayback Machine.: historia fupi ya Huntley na Palmers
  5. "Huntley & Palmers". Huntley & Palmers. [1] Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]