Howard W. Koch
Howard W. Koch | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Amezaliwa | Howard Winchel Koch Aprili 11, 1916 New York City, New York, USA | ||||||
Amekufa | 16 Februari 2001 (umri 84) Los Angeles, California, USA | ||||||
Ndoa | Ruth Koch (1937-2001) | ||||||
|
Howard Winchel Koch (11 Aprili 1916 - 16 Februari 2001) alikuwa mwongozaji na mtayarishaji wa filamu na televisheni kutoka nchini Marekani. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha filamu ya Ghost.
Alizaliwa mjini New York City, alihitimua katika shule ya Peddie School mjini Hightstown, New Jersey. Alianza shughuli za filamu akiwa kama mwajiriwa katika ofisi Universal Studios huko mjini New York halafu baadaye akaanza kutengeneza filamu za Hollywood kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1947 akiwa kama mwongozaji msaidizi. Alifanya kazi kama mtayarishaji kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1953 na mwaka mmoja baadaye akaanza kuongoza filamu kwa mara ya kwanza. Mnamo mwaka wa 1964, Paramount Pictures wakamchagua kuwa kama mkuu wa kitengo cha utayarishaji wa filamu, nafasi ambayo aliishikiria hadi hapo kunako mwaka wa 1966 pale alipoanzisha kampuni yake mwenyewe ya utayarishaji.
Viuno vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Howard W. Koch katika Find A Grave
- Howard W. Koch kwenye Internet Movie Database