Horace Campbell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Horace Campbell ni Profesa wa Sayansi ya Siasa na Masomo Kuhusu Wamarekani Weusi katika Chuo Kikuu cha Syracuse, New York. Campbell alizaliwa Montego Bay, Jamaika na kupata masomo yake Visiwa vya Karibi, Kanada, Uganda, na Uingereza. Kabla ya kuanza kufundisha Syracuse aliwahi kufundisha Chuo Kikuu cha Northwestern nchini Marekani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania.

Masomo yake ya udakitari aliyasomea kwenye Chuo Kikuu cha Sussex nchini Uingereza. Toka mwaka 1979 amekuwa akiandika na kufundisha kuhusu masuala ya jeshi na mabadiliko barani Afrika.

Horace Campbell ameshaandika na kuhariri vitabu mbalimbali. Kitabu chake maarufu ni kile cha Rasta and Resistance: From Marcus Garvey to Walter Rodney.


Familia[hariri | hariri chanzo]

Dr. Campbell amemuoa Professor Makini Zaline Roy, ambaye ni Profesa wa Elimu Chuo Kikuu cha Syracuse.

Machapisho[hariri | hariri chanzo]

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Makala[hariri | hariri chanzo]

Vipindi vya televisheni alivyoshiriki[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Horace Campbell kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.