Hifadhi ya Taifa ya Arli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hifadhi ya Taifa ya Arli, amara nyingi huitwa Arly, [1] ni mbuga ya taifa inayopatikana katika Mkoa wa Tapoa, kusini mashariki mwa Burkina Faso . [2] Inapakana na Mbuga ya taifa ya Pendjari ya Benin upande wa kusini na hifadhi ya Singou upande wa magharibi.

Jiografia na historia[hariri | hariri chanzo]

Maeneo Yanayolindwa ya IUCN na WAP

Hifadhi hiyo imewekwa katika kilomita za mraba 760 yenye aina mbalimbali za makazi ya viumbe, kama vile misitu ya hifadhi ya mito ya Arli na Pendjari na msitu wa savanna na vilima vya mchanga vya mnyororo wa Gobnangou.

Ni makazi ya takribani tembo 200 wa Kiafrika, viboko 200 na simba 100. Pia kuna nyati, nyani, tumbili wekundu na wa kijani kibichi, nguruwe, na swala wa aina mbalimbali, kama vile kore wa magharibi na swala roan . Pia kuna bushbucks, duiker na waterbuck . [3] [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Manson, K. (2006). "IV: The East", Burkina Faso. Bradt Travel Guides, The Globe Pequot Press Inc., 196. ISBN 1841621544. 
  2. Ouédraogo, O.; Schmidt, M.; Thiombiano, A.; Hahn, K.; Guinko, S.; Zizka, G. (2011). "Magnoliophyta, Arly National Park, Tapoa, Burkina Faso". Check List 7 (1): 85–100. https://biotaxa.org/cl/article/view/7.1.85.
  3. Manson, K. (2006). "IV: The East", Burkina Faso. Bradt Travel Guides, The Globe Pequot Press Inc., 196. ISBN 1841621544. Manson, K.; Knight (2006).
  4. UNEP Protected areas. UNEP and WCMC. 1984. http://www.unep-wcmc.org/protected_areas/data/sample/0113p.htm.
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Arli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.