Tapoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Tapoa katika Burkina Faso.

Tapoa ni wilaya katika Mkoa wa Mashariki nchini Burkina Faso. Wilaya hiyo iko mashariki kabisa mwa nchi hiyo. Wilaya imepokea jina lake kutokana na mto Tapoa unaopita humo.

Wilaya huwa na eneo la km² 14.572 na idadi ya wakazi kwenye mwaka 2013 ilikuwa 430,169[1].

Makao makuu yako mjini Diapaga. Miji mikubwa kiasi mbali na Diapaga ni Namounou na Tansarga. Wakazi wengi ni Wagourmanchema.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Annuaire statistique 2013 Archived 27 Februari 2015 at the Wayback Machine., kurasa 5–6, 22–23, 32–35