Nenda kwa yaliyomo

Msitu wa Amani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hifadhi ya Msitu ya Amani)
Chura wanaopatikana ndani ya msitu wa Msitu ya Amani

Msitu wa Amani ulioorodheshwa rasmi kama Hifadhi ya Msitu mwaka 1997 kwa ajili ya kulinda wanyama na uoto wa flora na fauna upande wa mashariki mwa Milima ya Usambara, Tanzania. Milima ya Usambara Mashariki na Magharibi ni sehemu muhimu kwa viumbe hai.

Hifadhi ya Mazingira ya Amani inajumuisha makazi ya misitu ya tropiki yenye mawingu.

Hifadhi hiyo kwa sasa imekuwa kivutio kizuri cha utalii kwani kimezidi kukua na kuongezeka.

Eneo hili la hifadhi lililopo Wilaya za Muheza na Korogwe katika Mkoa wa Tanga, lina makundi makubwa ya ndege, vipepeo na miti ambayo mingine hupatikana katika hifadhi hii tu. Pia kuna nyani weupe, weusi na wa rangi ya bluu.

Aina tisa za mimea jamii ya violet (African violet) na ndege kama bundi na tai Nduk Eagle owl ambao wanapatikana katika hifadhi hiyo pekee.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msitu wa Amani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.