Uoto wa Asili (Tanzania)
Mandhari
Uoto wa Asili ni mimea yote inayoota kiasili, tofauti na ile inayooteshwa na binadamu. Kwa hali hiyo uoto wa asili huhusiana moja kwa moja na tabia ya nchi. Kwa nchi ya Tanzania, tazama Tabia ya Nchi Tanzania.
Uoto wa asili ni matokeo ya athari za hali ya hewa, ambayo nayo huhusiana na kuathiriwa na sura ya nchi. Kwa mfano misitu minene hustawi katika sehemu za milima zenye mvua nyingi.
Aina na kiasi cha uoto wa asili hubadilika kadiri mvua inavyobadilika.
Aina za uoto wa asili Tanzania
[hariri | hariri chanzo]- Nyasi
- Misitu
- Mbuga
- Savanna ni nyasi na miti michache katika sehemu zenye mvua kidogo na ukame.
- Vichaka
- Java
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Vitabu vya Jiografia ya Tanzania
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uoto wa Asili (Tanzania) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |