Hamad bin Thuwain wa Zanzibar
Sayyid Hamad bin Thuwain Al-Buwsaid (kwa Kiarabu: حمد بن ثويني البوسعيد ; 1857 – 25 Agosti 1896) alikuwa Sultani wa tano wa Zanzibar. Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 5 Machi 1893 hadi 25 Agosti 1896.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Sayyid Hamad bin Thuwaini Al-Busaid yasemekana alizaliwa katika kisiwa cha Zanzibar mnamo mwaka 1857. Alimuoa binamu yake, Sayyida Turkia bint Turki, mtoto wa Turki bin Said, Sultani wa Muscat na Oman.
Sayyid Hamad bin Thuwain Al-Busaid alifariki ghafla tarehe 25 Agusti 1896 saa tano na dakika arobaini asubuhi, ikisemekana mara baada ya kupewa sumu na binamu yake Khalid bin Barghash ambaye alijitangaza kuwa sultani mpya baada ya kifo cha Sayyid Hamad akashikilia kiti hicho kwa siku tatu tu kabla ya kuondolewa na majeshi ya Waingereza katika vita vya Uingereza dhidi ya Zanzibar vilivyokuwa vya muda mfupi kabisa.[1].
Medali za Heshima
[hariri | hariri chanzo]- Italia: Grand Cross of the Order of the Crown of Italy (1893)
- Britania: Knight Grand Commander of the Order of the Star of India (1894)
- Ujerumani: Grand Cross of the Order of the Red Eagle, 1st Class (1895)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hernon, Ian (2003). Britain's Forgotten Wars. Stroud: Sutton Publishing. ku. 396–404. ISBN 978-0-7509-3162-5.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hamad bin Thuwain wa Zanzibar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |