Google Tensor
Google Tensor ni chip iliyotengenezwa na Google kwa ajili ya simu zake za Pixel, ikianza na Pixel 6. Chipu hii inaboresha utendaji wa simu kwa kuongeza uwezo wa Akili Bandia (Artificial Intelligence) na ML (Machine Learning. Tensor inaruhusu simu kufanya kazi nyingi za akili bandia kwa haraka na kwa ufanisi, kama vile uhariri wa picha na video, uchakataji wa lugha, na uwezo wa kuboresha usalama.
Chipu hii imeboreshwa zaidi na kufikia Tensor G4 katika Pixel 9 Pro, ikitoa kasi kubwa na utendaji mzuri zaidi wa Akili Bandia ikilinganishwa na vizazi vilivyotangulia. Tensor pia inasaidia kufanikisha sifa kama uhariri wa picha wa hali ya juu, utambuzi wa sauti, na uwezo wa kulinda data kwa msaada wa vipengele vya usalama vilivyojengewa ndani yake[1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |