Girlfriend (filamu)
Girlfriend | |
---|---|
Posta ya Girlfriend | |
Imeongozwa na | George Tyson |
Imetayarishwa na | Sultan Tamba Kessa Mwambeleko |
Imetungwa na | Sultan Tamba |
Nyota | TID |
Muziki na | P. Funk |
Imehaririwa na | Robert Kiata |
Imesambazwa na | GMC Wasanii Promoters |
Imetolewa tar. | 24, Mei, 2003 |
Nchi | Tanzania |
Lugha | Kiswahili |
Girlfriend ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2003 kutoka nchini Tanzania. Filamu inahusu muziki na maisha na ndani yake anakuja TID, Yvonne Cherrie (Monalisa), Beatris Morris (Nina), Jay Moe, A.Y na King Crazy GK. Filamu inaonesha jitihada binafsi katika kile unachokiamini na mwisho wa siku unatusua. Picha linaanza TID maisha magumu, harakati kila siku, huku ana mpenzi wake wa karibu mara kulala na njaa, mara hivi. Basi tu ilimradi maisha ya bahati nasibu. Hatimaye wakatoka katika namna ya kipekee licha ya majaribu kadhaa yaliyoonekana katika kipindi kigumu cha maisha yao. Filamu ina kibwagizo chake kinaitwa Girlfriend ambacho kiliimbwa na TID akishirikiana na Jay Moe kutoka Bongo Records.[1][2]
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Filamu inaanza Eric (T.I.D) akiwa nyumbani anasikiliza Sister Sister ya King Crazy GK kwa zogo kubwa. Ghafula Zuena (Yvonne Cherrie) anaingia kuzima mazogo yale. Zeuna anamsihi mpenziwe atafute kazi ya kufanya na si hiyo ya muziki. Eric anaamini katika muziki na kamwe hawezi kuacha muziki. Zuena anaona muziki hauna faida yoyote kwa Eric, kwani hata kodi inamshinda kulipa.
Mazungumzo yao hatimaye wakakubaliana kwenda ote katika kilabu ya muziki. Huko kilabuni, hakuwa kwenye ratiba, anabahatisha kutumbuiza. Kilabuni anaonekana Ndende, Jay Moe. Jahffarie, Sista P., G.K. anayebughudhi wasichana kilabuni hapo akiwa na A.Y. Stella (Nina) anamshawishi Zuena aachane na Eric kwa vile hana kitu. Bila mafanikio.
AY anamwona Zuena na kujaribu kumkuwadia GK. Eric bado hali mbaya katika kukubaliwa kutumbuiza. GK na AY wanarudi tena kuja kumbughudhi Zuena. Zuena anahofia nongwa na Eric na kuamua kuwatimua wawili wale. Kilabuni kunazuka ugomvi kila sehemu, GK na AY wanaleta fujo, hawataki kulipa pesa za vinywaji walivyokunywa. Hadi mwisho, Eric kabaniwa kutumbuiza kule kilabuni. Nyumbani kwa GK kinanuka kati ya Stella na mwanamke mwengine (Joan). GK kagonganisha magari.
Nyumbani kwa Sam (kakake Eric), malumbano makubwa ndani ya nyumba. Amekuwa kisirani kiasi hata mkewe anaoiona hiyo hali.
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Wimbo wa Girlfriend katika YouTube
- ↑ Girlfriend Archived 30 Mei 2013 at the Wayback Machine. katika Bongo Cinema.com
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Girlfriend (filamu) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |