Sultan Tamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sultan Tamba ni muongozaji na pia mtunzi wa filamu kutoka nchini Tanzania. Yeye ni miongoni mwa watayarishaji wa mwanzo waliosaidia kuhamasisha upya utengenezaji na utazamaji wa filamu za Kitanzania kwa kutunga na kutayarisha filamu ya Girlfriend. Filamu hiyo aliitayarisha kwa kusaidiana na rafiki yake Kessa Mwambeleko na Eric Shigongo na kuongozwa na Mkenya, George Tyson. Baada ya hapo, alitunga filamu nyingine nyingi na kuziongoza mwenyewe. Sultan Tamba anatoka katika ukoo wa wenye vipaji maalum vya filamu. Kaka yake Dk. Maneno Tamba pia ni mtengeneza filamu.

Filamu ambazo amezitengeneza hadi sasa ni Girlfriend, Siri. Bosi, Mzee wa Busara (Part I & II), Noti, Shetani wa Mahaba, Jinamizi, Roho Mbili, Pete, Bestfriend, Kazibure Village, Wasiwasi, Sumu ya Moyo, Chozi la Damu, Miwani Meusi, In the House, Kisu na Soka la Bongo.

Kuanzia mwaka 2008, Tamba alijiunga na masomo ya film animation kwenye chuo kiitwacho Media One School of Digital Animation cha mjini Dar es Salaam na kumaliza masomo hayo mwaka 2009 Mei ambapo alichukua fani ya 3D animation & Motion Graphics. Ndio kuwema kwamba hivi sasa mbali na filamu za kawaida, pia ana uwezo wa kutengeneza filamu za katuni za Digital 3D.

Malengo yake ni kujiunga na masomo ya juu zaidi ya mambo hayo ya 3D animation kwa mwaka 2010.

Filamu yake ya mwisho inaitwa Sanda Nyeusi na imetoka mwezi Septemba 2009.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sultan Tamba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.