George Mcheche Masaju

George Mcheche Masaju (alizaliwa 7 Aprili 1965) ni mwanasheria na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania wa tisa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama baada ya Jaji Mkuu wa Sita Mzalendo Prof. Ibrahim Hamis Juma kustaafu kwa mujibu wa Sheria[1]. Mwaka 2015 aliteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi akaendelea katika nafasi hii baada ya kuingia kwa raisi mpya John Magufuli.[2][3]
Masaju alikuwa mshauri wa kisheria katika ofisi ya raisi kabla ya kuwa naibu mwanasheria mkuu mwaka 2009. [4] . Kutoka hapo alipanda cheo baada ya kujiuzulu kwa mwanasharia mkuu aliyetangulia.
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]George Mcheche Masaju alizaliwa tarehe 7 Aprili 1965 katika kijiji cha Bwai, Wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania. Alianza elimu yake nchini Tanzania, akipitia ngazi mbalimbali za masomo hadi kufikia elimu ya juu katika taaluma ya sheria. Miaka yake ya awali iliundwa na nidhamu ya kielimu pamoja na mfumo wa elimu wa Tanzania, ambao ulimwandaa kwa maisha ya utumishi wa umma na sheria.
Baada ya kuhitimu masomo yake rasmi, Masaju alianza kazi serikalini kama Wakili wa Serikali mnamo Aprili 1994. Alihudumu katika nafasi mbalimbali za juu za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwa Mshauri wa Kisheria wa Rais na baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Msingi wake thabiti wa kielimu na kujitolea kwake katika misingi ya sheria vilichangia katika taaluma yake mashuhuri katika mfumo wa sheria wa Tanzania.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "RAIS SAMIA AMTEUA JAJI GEORGE MCHECHE MASAJU KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA". www.jsc.go.tz. JSC. Iliwekwa mnamo 2025-06-14.
- ↑ "Rais amteua George Mcheche Masaju kuwa Mwana Sheria Mkuu wa Serikali". Michuzi Blog. 3 Januari 2015. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Masaju sworn in as Attorney General". Iliwekwa mnamo 2016-10-12.
- ↑ "JK kuapisha aliowateua leo". Michuzi Blog. 21 Oktoba 2009. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George Mcheche Masaju kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |