George Floyd
George Floyd (1973 - 25 Mei 2020) alikuwa Mmarekani Mweusi kutoka Minnesota aliyefariki dunia kufuatia askari polisi mweupe wa Minneapolis, aliyejulikana kwa jina la Derek Chauvin[1] kumbana Floyd kwa kupiga goti juu ya upande wa nyuma wa shingo ya Floyd kwa muda wa takribani dakika 8 na sekunde 46 kadiri ya maelezo yaliyomo kwenye faili la malalamiko ya jinai lilofunguliwa dhidi ya Chauvin.[2][3].
Kifo chake
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 25 Mei, 2020, George Floyd aliuawa katika jiji la Minneapolis nchini Marekani na Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu mwenye umri wa miaka 44.[4] Floyd alikamatwa kwa tuhuma za kutumia noti ghushi ya $20. Chauvin alipiga magoti kwenye shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa huku Floyd akiwa amefungwa pingu na kulala kifudifudi barabarani.[5][6][7] Maafisa wengine wawili wa polisi, J. Alexander Kueng na Thomas Lane, walimsaidia Chauvin kumzuia Floyd.[8] Lane pia alikuwa ameelekeza bunduki kwenye kichwa cha Floyd kabla ya Floyd kufungwa pingu. Afisa wa nne wa polisi, Tou Thao, aliwazuia watu waliokuwa karibu na eneo hilo kuingilia kati.[9]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.washingtonpost.com/nation/2020/05/29/officer-charged-george-floyds-death-used-fatal-force-before-had-history-complaints/ Jarida la Washingpost, liliangaliwa 03 June 2020
- ↑ https://edition.cnn.com/us/live-news/george-floyd-protest-updates-05-28-20/h_d6de512e51a8858a57f93ffa732c2695
- ↑ https://www.mediaite.com/uncategorized/officials-say-derek-chauvin-had-knee-on-george-floyds-neck-for-almost-3-minutes-after-floyd-was-unresponsive/
- ↑ "Derek Chauvin found guilty of murder of George Floyd". the Guardian (kwa Kiingereza). 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2022-04-16.
- ↑ https://www.bbc.com/news/world-us-canada-52861726
- ↑ Barker, Kim; Eligon, John; Jr, Richard A. Oppel; Furber, Matt (2020-06-04), "Officers Charged in George Floyd's Death Not Likely to Present United Front", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2022-04-16
- ↑ Barker, Kim; Eligon, John; Jr, Richard A. Oppel; Furber, Matt (2020-06-04), "Officers Charged in George Floyd's Death Not Likely to Present United Front", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2022-04-16
- ↑ https://www.youtube.com/watch?v=WcGtHFluijI&feature=youtu.be
- ↑ Chappell, Bill (2020-06-03), "Chauvin And 3 Former Officers Face New Charges Over George Floyd's Death", NPR (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-04-16
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George Floyd kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
[[Jamii:{{ #if:1973|Waliozaliwa 1973|Tarehe ya kuzaliwa