Nenda kwa yaliyomo

George Abbott (mwanasoka)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

George Benedict Abbott (alizaliwa 17 Agosti 2005) ni raia wa Uingereza mcheza kandanda la kulipwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs kama kiungo wa kati.

Safari ya Kandanda

[hariri | hariri chanzo]

Abbott ni zao la Tottenham Hotspurs tangu akiwa na umri wa miaka saba. Alisaini mkataba wake wa kwanza kama mchezaji wa kulipwa na klabu tarehe 15 mwezi wa 3 mwaka 2023.[1]  alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya wakubwa akitokea benchi kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza mchezo dhidi ya Leeds United wakishinda 4-1 ilikuwa tarehe 28 mwezi wa 5 mwaka 2023.[2]

Msimu wa 2023-24, Abbott alikuwa kapteni wa kikosi cha Tottenham Hotspurs vijana umri chini ya miaka 21 na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya vijana.[3]

Timu ya Taifa

[hariri | hariri chanzo]

Abbott mchezaji wa kimataifa wa Uingereza, akiwa ameichezea timu ya taifa vijana umri chini ya 18.[4]

Aina yake ya uchezaji

[hariri | hariri chanzo]

Abbott ni mchezaji hodari ambaye kimsingi ni kiungo mkabaji. Anaweza pia kucheza safu ya nyuma kama beki wa kati, msimu wa 2022-23 alicheza kama beki wa kulia. [5] Ni mchezaji shupavu na mwenye kasi, na anauwezo wa kucheza eneo kubwa uwanjani.[6]

  1. "First professional contract for Abbott". Tottenham Hotspur (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-03.
  2. https://www.skysports.com/football/news/11095/12886941/leeds-1-4-tottenham-harry-kane-nets-twice-to-relegate-leeds-from-premier-league-but-spurs-miss-out-on-europe
  3. https://www.premierleague.com/match/115685/premier-league-2/2023-24/spurs-u21-v-sunderland-u21
  4. https://www.englandfootball.com/articles/2023/Mar/22/england-mens-under-18-croatia-match-report-20230322
  5. https://www.football.london/tottenham-hotspur-fc/players/talented-tottenham-wonderkids-daniel-levy-26867652
  6. https://superhotspur.com/2022/07/28/my-piece-on-talented-and-versatile-spurs-academy-player-and-second-year-scholar-george-abbott/