Nenda kwa yaliyomo

Kambu-ardhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Geobiastes)
Kambu-ardhi
Kambu-ardhi kichwa-buluu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Coraciiformes (Ndege kama viogajivu)
Familia: Brachypteraciidae (Ndege walio na mnasaba na kambu-ardhi)
Jenasi: Atelornis Pucheran, 1846

Brachypteracias Lafresnaye, 1834
Geobiastes Sharpe, 1871
Uratelornis Rothschild, 1895

Spishi: Angalia katiba

Kambu-ardhi ni ndege wa familia Brachypteraciidae wanaotokea Madagaska tu. Wanafanana na viogajivu wadogo lakini hawana rangi kali, isipokuwa kichwa cha kambu-ardhi kichwa-buluu na kile cha kambu-ardhi kichwa-chekundu. Hutafuta chakula chini na hula wadudu na watambaachi. Tago lao ni kishimo ardhini. Jike huyataga mayai 1-4.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]