Gdansk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera
Gdansk - Danzig : Mji wa Kale

Gdańsk (Kijerumani: Danzig) ni mji wa bandari katika kaskazini ya Poland pale ambako mto Vistula unaishia katika Bahari Baltiki. Mji una wakazi wapatao 500,000 na kuna bandari muhimu zaidi ya Poland.[1]

Mji ukikuwepo tayari mnamo mwaka 900 BK na tangu mwaka 979 eneo lake liliingizwa mara ya kwanza katika milki ya Poland. Katika karne ya 13 mtemi Swantopolk alikaribisha walowezi Wajerumani kuanzisha mji chini ya utaratibu wa kwao nyumbani. Mji huu wa Kijeurmani ulikua na kuwa mju muhimu wa biashara na tasnifu ikaungana na makazi ya awali wa wazalendo. Mji wa Danzig (jina la Kijerumani) uliendelea kuwa mji wa utamaduni wa Kijerumani lakini kwa karne kadhaa ilikuwa mji wa kujitawala chini ya Dola la Wamisalaba Wajerumani na baadaye chini ya mfalme wa Poland. Baada ya magawio ya Poland ilikuwa mji wa Prussia tangu 1796 na baadaye mji katika Ujerumani. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Danzig ilitengwa na Ujerumani na kuwa Dola-mji hadi kuvamiwa na Ujerumani 1939. Mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1945/46 wakazi Wajerumani walifukuzwa na mji wote pamoja na mashariki ya Ujerumani ilikuwa sehemu ya Jamhuri ya Poland. Sasa jina lake ni Gdansk.

Mji ulioharibika sana vitani ikajengwa upya kwa kuiga majengo ya awali. Katika miaka ya utawala wa kikomunisti katika Poland Gdansk iliendelea kuwa kitovu cha upinzani na mahali ambako chama cha Solidarnocz kilianzishwa.

References[hariri | hariri chanzo]

  1. About Port. Port of Gdansk Authority. Iliwekwa mnamo 2009-11-05.