Gazi Yasargil

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mahmut Gazi Yaşargil (amezaliwa Julai 6, 1925) ni daktari wa Uturuki anayejishughulisha na upasuaji wa ubongo. Yaşargil alitibu wagonjwa wa kifafa na uvimbe wa ubongo kwa kutumia vifaa alivyoviunda yeye mwenyewe.

Kuanzia 1953 hadi kustaafu kwake mnamo 1993 alikuwa mkazi wa kwanza, mkazi mkuu na kisha profesa na mwenyekiti wa Idara ya upasuaji wa ubongo, Chuo Kikuu cha Zurich na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Zurich.

Mnamo mwaka wa 1999 aliheshimiwa kama "Neurosurgery’s Man of the Century 1950–1999" kwenye Mkutano wa Mwaka wa madaktari wapasuaji wa Ubongo. Yeye ni mwanachama mwanzilishi wa Chuo cha Ulaya.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gazi Yasargil kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

}