Nenda kwa yaliyomo

Ganga (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Ganga (Ganges)
Ramani ya Beseni ya mto Ganga
Ramani ya Beseni ya mto Ganga
Chanzo barafuto ya Gangotri
Mdomo Ghuba ya Bengali
Nchi za beseni ya mto India, Bangladesh
Urefu 2,510 km
Kimo cha chanzo 7,756 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 14,270 m³/s
Eneo la beseni (km²) 907,000 km²
Mjini Varanasi kuna mahekalu mengi kando la mtoni

Ganga (Kisanskrit गङ्गा, gaṅga) ni mto mkubwa katika Uhindi wa Kaskazini. Mto una uefu wa 2,511 km unapita nchi za Uhindi na Bangla Desh (Asien).

Chanzo chake ni katika milima ya Himalaya inapokutana mito ya Alaknanda na Bhagirathi. Kutoka hapa inaendelea kuelekea kusini-mashariki hadi tambarare ya Bengali. Nchini Bangla Desh inaunganika na mto Brahmaputra na kuwa na delta kubwa hadi kuingia katika Bahari Hindi.

Ganga na dini

[hariri | hariri chanzo]

Katika imani ya Uhindu Ganga ni mto mtakatifu. Huabudiwa pia kama mungu wa kike. Wafuasi wa dini ya Uhindu mara nyingi wanajaribu kuhiji mtoni kabla ya kufa wakitumaini ya kwmaba maiti itachomwa na majivu kumwagika mtoni. Kuoga mtoni kunatazamiwa kama bafu ya kuondoa dhambi.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ganga (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.