Fudi
Mandhari
Fudi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fudi mwekundu (Foudia madagascariensis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 6:
|
Fudi (kutoka Kimalagasi: fody) ni ndege wadogo wa jenasi Foudia katika familia Ploceidae ambao wanatokea Madagaska na visiwa vingine katika Bahari ya Hindi. Ndege hawa ni wakubwa kuliko kwera na wakati wa kuzaa madume wana nyekundu au njano kichwani na pengine sehemu nyingine za mwili. Spishi nyingine hula mbegu hasa, nyingine hula wadudu hasa. Hulifuma tago lao kwa manyasi na majani na hulining'inizia kitawi au jani kubwa. Jike huyataga mayai 2-3.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Foudia aldabrana, Fudi wa Aldabra (Aldabra Fody)
- Foudia delloni, Fudi wa Reunion ( Réunion Fody) – imekwisha sasa (baada ya 1672)
- Foudia eminentissima, Fudi Kichwa-chekundu (Comoros au Red-headed Fody)
- Foudia flavicans, Fudi wa Rodrigues (Rodrigues Fody)
- Foudia madagascariensis, Fudi Mwekundu (Red Fody)
- Foudia omissa, Fudi-misitu (Forest Fody)
- Foudia rubra, Fudi wa Morisi (Mauritius Fody)
- Foudia sechellarum, Fudi wa Shelisheli (Seychelles Fody)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Fudi-misitu
-
Fudi wa Morisi