Frasila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Frasila (pia farasila, frasla; asili ya kiar.) ni kipimo cha uzito wa takriban 16 kg.

Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili si kipimo sanifu cha kisasa.

Zamani za biashara ya misafara "frasila" ilikuwa kipimo cha kawaida cha kupima kiasi cha mzigo fulani. Mara nyingi frasila kilitajwa kama kipimo cha pembe ya ndovu.

Mfano:[hariri | hariri chanzo]

"Wakati huu Urori frasila ya ushanga kwa frasila ya pembe, nguo thenashara ila khamstashara kwa frasila, bizari frasila kwa frasila, sanduku ya sabuni kwa frasila ya pembe, baruti khamstashara ratli kwa frasila" (Maisha ya Hamed bin Muhammed el Murjebi yaani Tippu Tip kwa meneno yake mwenyewe, EALB 1974 § 16, uk. 20)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]