Frans Claerhout

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Frans Claerhout (15 Februari 1919 – 4 Julai 2006) alikuwa mchoraji wa Ubelgiji ambaye alitumia muda mwingi wa maisha yake nchini Afrika Kusini .

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Claerhout alizaliwa huko Pittem, West Flanders mnamo 1919, na kuhamia Afrika Kusini kama mmisionari wa Kanisa Katoliki mnamo 1946, akiwa na umri wa miaka 27. Alihama baada ya kumaliza mafunzo yake ya ukuhani. Wadhifa wake wa kwanza ulikuwa Transvaal mnamo mwaka 1948 na baadae alihamishiwa katika Jimbo la Orange Free State. [1] Alifanya kazi karibu na Bloemfontein katika jimbo la Free State la Afrika Kusini. Alifanya kazi ya ukuhani na kwa muda wake wa ziada alijikita kwenye sanaa. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 2013 "Father Frans Claerhout 1919 – 2006" Accessed 22 August.
  2. "SA Artist, Father Frans Claerhout, is born". South African History Online. Iliwekwa mnamo 30 July 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Frans Claerhout kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.