Felice Albers
Mandhari
Felice Albers. (amezaliwa 27 Desemba 1999)[1] ni mchezaji wa magongo katika uwanja wa Uholanzi.[2]
Klabu alizochezea
[hariri | hariri chanzo]Albers anacheza mpira wa magongo katika klabu ya Amsterdam iliyopo nchini ya Uholanzi[3][4]. Mnamo 2019, Albers alikuwa mshiriki wa timu ya Amsterdam ambayo ilishinda Kombe la 47 na la mwisho la Klabu Bingwa ya mpira wa magongo. Katika fainali timu ilishinda 7-0 dhidi ya Real Sociedad katika dimba la Amstelveen, Uholanzi.[5] Mnamo 2016, Albers aliwakilisha timu ya chini ya umri wa miaka18 ya Uholanzi kwenye Mashindano ya Vijana ya Ulaya ya mpira wa magongo. Katika mashindano hayo, alifunga goli moja na kushinda medali ya dhahabu na timu yake.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://tms.fih.ch/competitions/1064/reports/teams
- ↑ "International Hockey Federation". tms.fih.ch. Iliwekwa mnamo 2021-12-04.
- ↑ "AH & BC". www.ahbc.nl. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-04. Iliwekwa mnamo 2021-12-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-23. Iliwekwa mnamo 2021-12-04.
- ↑ "European Hockey Federation: Altiusrt". eurohockey.altiusrt.com. Iliwekwa mnamo 2021-12-04.
- ↑ "European Hockey Federation: Altiusrt". eurohockey.altiusrt.com. Iliwekwa mnamo 2021-12-04.