Farzaneh Fasihi
Mandhari
Farzaneh Fasihi (Kifarsi: فرزانه فصیحی; alizaliwa Isfahan, 1993) ni mwanariadha wa mbio fupi kutoka nchini Iran. Aliwakilisha nchi yake katika mashindano zaidi ya 10 ya barani Asia. Fasihi anashika wa rekodi ya Iran ya mita 60 ndani ya ukumbi kwa sekunde 7.25.
Alishiriki kimataifa mara ya kwanza kwenye Mashindano ya Riadha ya Ukumbini ya Asia ya 2016 huko Doha, ambapo alimaliza kwenye nafasi ya 5 katika 60 m na katika 4 x 400 mbio wa rilei alifikia medali ya fedha.
Mwaka 2018 Fasihi alikuwa mbingwa wa Iran wa mbio wa mita 100 na mbingwa wa mita 60 ukumbini. Aliwakilisha Iran kwenye mbio wa wanawake mita 100 wakati wa Michezo ya Olimpiki mwaka 2020 akimaliza kwa sekunde 11.79[1].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ FARZANEH Fasihi Archived 2 Oktoba 2021 at the Wayback Machine., tovuti ya Olimpiki 2020