Nenda kwa yaliyomo

Faras

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Faras likiwa ndani ya Nubia (juu kushoto)
Fresco ndani ya kanisa
Capital from Faras (London, British Museum)
St. Anne, the fresco katika makumbusho ya Faras (National Museum, Warsaw)

Faras (zamani waliita kwa Kigiriki Παχώρας, Pakhôras; Latin: Pachoras; Kinubi cha Kale: Ⲡⲁⲣⲁ, Para) ulikuwa moja kati ya miji mikubwa ya Lubia ya upande wa chini, katika Misri ya leo. Mji huu ulifurika na mafuriko ya Ziwa Nasser katika miaka ya 1960, na sasa mji huu upo chini ya maji kwa kudumu. Kabla ya mafuriko, wana-elimu wa kale walifanya utafiti mkubwa sana katika eneo hili. Wanaelimu wa kale hao walitokea nchini Poland.

Kwa kurudi nyuma katika kipindi cha kwanza, kipindi ambacho mji wa Faras ulikuwa mji mkubwa sana, hususani katika kipindi cha Meroe jamii ya watengenezaji zana za chuma. Eneo hili lilikuwa kama hekalu. Katika kipindi cha Wamisti kutaka kuongoza eneo la Nubia aneo la Faras lilikuwa ndilo eneo la uongozi wa utawala wa Wamisri, ambao ulikuwa katika maeneo ya ukanda wa juu kuanzia katika eneo la Abu Simbei, ambapo hata utamaduni wa Misri ulikuwa umeenea sana.

Jiji hili, lilizidi kupata umaarufu katika kipindi cha Wakristu wa Nubia, wakati mji wa Faras ulikuwa ni mji mkuu wa miji ya Basiliskos Silko wa Nobadia. Wakati mji wa Nobatia ulipomezwa na Makuria mji wa Faras ulibaki kuwa maarufu katika upande wa Kaskazini, na kuchukua nafasi ya Nobadia. Moja kati ya ugunduzi mkubwa uliofanywa katika kipindi hiki ni ugunduzi wa kanisa la kikristu la mji huo. Kanisa hili, lilikuwa limemezwa na mchanga nah ii ukalifanya kuendelea kutunza rangi na michoro mbalimbali katika kuta zake.

Michoro hii, ni moja ya mifano hai ya kuwepo kwa sanaa ya Wakristu wa Nubian. Walichonga na kuchoro mbalibali hususani kuhusina na biblia na mapadri mbalimbali wa eneo hilo. Michoro hiyo imetuzwa hadi leo na ipo katika maonesho katika eneo la Warsaw na Khartoum. Na pia kuna mashairi yaliypatikana katika eneo la Faras

Katika miaka ya hivi karibuni, Wakristu kutoka Nubia, Faras wanaonekana kuanguka nahata ofisi za utawala zimeamishiwa katika sehemu iliyo rahisi zaidi kufikika ya Qasr Ibrim.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

[[http://web.archive.org/20081216072305/http://www.khm.at/faras/framesetE.html Ilihifadhiwa 16 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine. Exhibition on Faras]], Vienna 2002 [Medieval Nubia]