Esther Dang
Esther Dang (alizaliwa 5 Machi 1945) ni mwanauchumi kutoka nchini Cameroon.
Alijiuzulu kama mkurugenzi wa kampuni ya uwekezaji ya Cameroon ili kugombea urais. [1]
Maisha na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Dang alizaliwa Mbalmayo mwaka 1945 [2]. Alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Yaoundé mwaka 1966 hadi 1969 na baadae kuendelea masomo yake katika Chuo Kikuu cha Grenoble ambako aliendelea kusoma uchumi na hatimae alihitimu mwaka 1971[3]. Dang ana udaktari katika uchumi kutoka Sorbonne[4].
Alipandishwa cheo na René Owona, ambaye alikuwa waziri wa maendeleo ya viwanda, akiongoza kama mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Uwekezaji ya Cameroon Société nationale d'investissement du Cameroun mnamo 1 Oktoba 1990. [5] Owena na Simon Ngann Yonn , ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, wote walikufa mwaka 2004.
Alikuwa mkurugenzi mkuu na alijiuzulu kutoka nafasi hii katika mzozo ulioambatana na hasira. Nafasi yake ilichukuliwa na Yaou Aïssatou ambaye alikuwa waziri wa wanawake
Alikuwa mgombea wa urais nchini Cameroon mwezi Oktoba 2011. Alikuwa mmoja wa wanawake watatu waliojitokeza kama wagombea. Mwingine alikuwa Edith Kahbang Walla, lakini wagombea wakuu walikuwa Paul Biya na Ni John Fru Ndi. Kulikuwa na wagombea 50 na Paul Biya alichaguliwa tena kwa wingi mkubwa katika uchaguzi wa rais wa Cameroon wa 2011. Dang alishika nafasi ya 11 akiwa na asilimia 0.33 ya kura.
Mwaka 2016 Dang alituma barua ya wazi kwa rais kufuatia kukatika kwa treni ya Eséka mwaka 2016 iliyosababisha vifo vya watu kadhaa na kuzuia usafiri wowote kuingia katika miji miwili mikubwa nchini Cameroon. Barua hiyo iliuliza maswali mengi kuhusu rekodi ya rais na mipango yake ya siku zijazo. Maswali mengi ni pamoja na "Kwa nini unakataa kuiendeleza Cameroon?" na "Ni nini kwa maoni yako ni lengo la Mkuu wa Nchi?"
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Quick facts for kids Esther Dang with awards Born March 5, 1945 Mbalmayo Nationality Cameroonian Occupation Economist Employer National Investment CompanyKnown for director general of the National Investment Company. "Esther Dang Facts for Kids". kids.kiddle.co (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-08-25.
{{cite web}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Korff-Sausse, Simone (2019-01-18). "Un corps qui fait du bruit : le cri dans la peinture". Corps & Psychisme. N° 73 (1): 193–196. doi:10.3917/cpsy2.073.0193. ISSN 2496-4476.
{{cite journal}}
:|volume=
has extra text (help); no-break space character in|title=
at position 27 (help) - ↑ Baticle, Christophe; Boutinot, Laurence (2021-07-01). "Parcours d'une résistance silencieuse dans les forêts du Cameroun". Cahiers d'Outre-Mer. 74 (284): 383–415. doi:10.4000/com.13294. ISSN 0373-5834.
- ↑ Korff-Sausse, Simone (2019-01-18). "Un corps qui fait du bruit : le cri dans la peinture:". Corps & Psychisme. N° 73 (1): 193–196. doi:10.3917/cpsy2.073.0193. ISSN 2496-4476.
{{cite journal}}
:|volume=
has extra text (help) - ↑ Mens, Yann (2018-11-01). "Au Cameroun, Paul Biya remet le couvert". Alternatives Économiques. N° 383 (10): 38–38. doi:10.3917/ae.383.0038. ISSN 0247-3739.
{{cite journal}}
:|volume=
has extra text (help)