Esteri Tebandeke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Esteri Tebandeke

Esteri Tebandeke (alizaliwa 16 Mei 1984) ni mwigizaji wa filamu, mwanamuziki na msanii aliyejulikana nchini Uganda.

Alihitimu katika shule ya Margret Trowell ya viwanda na sanaa katika chuo kikuu cha Makerere. Alishiriki katikafilamu zilizojulikana kwa majina ya Sins of the parents 2008, Master on Duty 2009, Queen of Katwe2006 na Her Broken Shadow 2016.

Maisha ya awali na elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Esteri ni mzaliwa wa Kampala, nchini Uganda. Ni mtoto wa sita kati ya watoto nane katika familia yake. Familia yake walikua wakiishi nchini Uganda. Esteri alihudhuria shule ya sekondari ya wasichana St Joseph nchini Uganda, na alikua akishiriki kucheza miziki shuleni.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Esteri alianza kufanya kazi kama mwanamziki mwaka 2008 and alishiriki kwenye kampuni nyingi za kimziki nchini Uganda zilizojulikana kama Keiga Dance Company, Stepping Stones dance company, Mutumizi dance Company, Guerrilla Dance Company na mengine mengi. Alishiriki kutumbuiza kwenye majukwaa mbalimbali kama vile Dance Week Uganda, Dance Transmissions Festival, Bayimba International Festival of the Arts and Umoja International Festival akiwa kama mwanafunzi na akiwa mwalimu kwa miaka mitatu. Hakua anafanyia kazi yake Uganda tu bali pia alishiriki kwenye miradi mbalimbali ya kisanaa nchini Kenya, Rwanda,Madagascar, south Africa, Tanzania,Marekani,na Ethiopia. Alitumbuiza kwenye La Mama nchini New York mwaka 2012, Artwater village Theatre mwaka 2013 na katika New Orleans Fringe mwaka 2014. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Esteri Tebandeke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.