Nenda kwa yaliyomo

Esmé Frances Hennessy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Esmé Frances Hennessy

Dr. E. F. Hennessy
Amezaliwa Agosti 1933
Umzinto
Nchi Afrika Kusini
Kazi yake Mtaalamu wa mimea, Mchoraji na Mwandishi


Esmé Frances Hennessy, née Franklin (amezaliwa Umzinto, Agosti 1933) ni mtaalamu wa mimea, mchoraji wa mimea na mwandishi wa Afrika Kusini.

Aliandika kuhusu maua ya Afrika ya Kusini yajulikanayo kama Erythrinas (South African Erythrinas) mwaka 1972, Orchids of Africa 1961akishirikiana na Joyce Stewart, The Slipper Orchids 1989 akishirikiana na Tessa Hedge na Flowering plants of Africa.[1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Esmé Franklin alizaliwa katika familia ya daktari. [1] Alijifunza elimu ya mimea na wanyama katika chuo kikuu cha Natal na kupata shahada ya uzamivu ya elimu ya mimea mwaka 1983.[2]

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Kutokea mwaka 1958 mpaka 1960 aliajiriwa kama msaidizi wa tafiti katika kituo cha tafiti cha “C.S.I.R. Amoebiasis Research Unit”. [3] Mwaka 1961 Hennessy alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Durban- Westville.[4] [1]

Mwaka 1972 Hennessy alichapisha kitabu kiitwacho South African Erythrinas.[3] alitengeneza maonyesho mbali mbali na maelezo juu ya mimea ya Afrika (Flowering Plants of Africa) na kushirikiana katika uandishi wa Orchids of Africa (1981) akiwa na Joyce Stewart, The Slipper Orchids (1989) akiwa na Tessa Hedge.[2] Alifanya maonyesho ya kimataifa naya ndani ya nchi ikiwepo “Hunt Institute for BotanicalDocumentation|Hunt Institute” iliyofanyika Pittsburgh, USA mwaka 1977, akionyesha mimea inayopatikana kusini mwa Afrika. [5] Alifanya maonyesho pia katika Royal Horticultural Society, Uingereza mwaka 1989 na 1992 na kuzawadia medali mbili za shaba na kushiriki katika maonyesho ya Smithsonian Institution ya Washington mwaka 2000.[2]

Hennessy alistaafu kutoka katika idara ya mimea cha chuo kikuu cha Durban-Westville mwaka 1993 na kwa sasa ni profesa katika shule ya mime ana Wanyama cha chuo kikuu cha Natal, Pietermaritzburg.[6] Mnamo mwaka 2012, Henessy alielezea kitabu kiitwacho Beautiful Corn: America’s Original Grain from Feed to Plate iliyoandikwa na Anthony Boutard.[7]

Kazi zake alizoziandika na kushirikishwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Clinical amoebiasis iliyoandikwa na Alexander Joseph Wilmot (1962)
  • South African Erythrinas iliyoandikwa na Esmé Franklin Hennessy (1972)
  • Orchids of Africa: a select review iliyoandikwa na Joyce Stewart (1981)
  • The slipper orchids iliyoandikwa na Esmé Franklin Hennessy (1989)
  • Of rushes, resources and riots iliyoandikwa na Esmé Franklin Hennessy (2000)
  • Terrestrial African orchids: a select review iliyoandikwa na John S Ball (2009)
  1. 1.0 1.1 1.2 "BAASA Newsletter [[2009]] No 2_processed.pdf". Botanical Art Association of Southern Africa. Juni 2009. Iliwekwa mnamo 2021-02-10. {{cite web}}: URL–wikilink conflict (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Botanical Artists Association of Southern Africa: Esmé Hennessy". Botanical Artists Association of Southern Africa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-23. Iliwekwa mnamo 2021-02-10.
  3. 3.0 3.1 Gunn, Mary; Codd, L. E. W. (1981-06-01). Botanical Exploration Southern Africa (kwa Kiingereza). CRC Press. uk. 182. ISBN 978-0-86961-129-6.
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named :1
  5. "Hunt Institute International Art Exhibition" (PDF). The Council on Botanical and Horticultural Libraries. Oktoba 1977. Iliwekwa mnamo 2021-02-10.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  6. "Editorial" (PDF). Journal of the Natal Society. 20: 5. Desemba 2000.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Boutard, Anthony (2012-09-01). Beautiful Corn: America's Original Grain from Seed to Plate (kwa Kiingereza). New Society Publisher. ISBN 978-1-55092-522-7.