Nenda kwa yaliyomo

Escopetarra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Escopetarra inayoonyeshwa kwenye jengo la UM mjini New York

Escopetarra ni gitaa iliyotengeneza na bunduki inayotumika kama ishara ya amani. Jina limeundwa kutokana na maneno mawili Kihispania escopeta (bunduki) na guitarra (gitaa).[1]

Escopetarra ilibuniwa na mwanaharakati wa Kolombia César López kwenye mwaka 2003[2]. Kiasili alitengeneza nakala tano alizokabidhi kwa rafiki zake waliokuwa wanamuziki Juanes na Fito Páez, halafu Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Jiji la Bogota. Nakala moja aliyobaki nayo aliuza baadaye kwa $ 17,000 kwenye mkutano wa kuchangia pesa kwa wahanga wa mabomu ya ardhini[3].

Nakala ya escopetarra iliyopewa kwa UNDP ilionyeshwa kenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu upunguzaji wa silaha za vita duniani[4]. Baadaye imeonyeshwa hadharani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "MAKE: Blog: Guitar made from AK-47 - The Escopetarra". web.archive.org. 2007-01-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-25. Iliwekwa mnamo 2022-08-16.
  2. Making music out of menace: A Colombian musician has fashioned guitars out of rifles to help spread a message of peace. Miami Herald, March 7, 2006
  3. Latorre, Héctor. "Escopetarras: disparando música", BBC World, 2006-01-24. Retrieved on 2007-01-31. 
  4. Conte, Gabriel. "La escopeta transformada en guitarra del músico César López será exhibida en la ONU", Desarme.org, 2006-06-15. Retrieved on 2007-01-31. Archived from the original on 2007-09-29.