Nenda kwa yaliyomo

Erin Phillips

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Erin Phillips

Erin Phillips (alizaliwa Melbourne, 1985) ni mwanamichezo kutoka Australia aliyejipatia umaarufu kwa mafanikio katika mpira wa kikapu na mpira wa miguu wa Australia (AFLW).

Baba yake alikuwa mchezaji maarufu wa mpira wa miguu. Alianza na mpira wa kikapu, akishinda medali ya dhahabu kwenye Mashindano ya Dunia ya mwaka 2006 na medali ya fedha kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008[1][2].

Mwaka 2017, alihamia AFLW na kuchezea Adelaide Crows, ambako alishinda tuzo ya mchezaji bora mara mbili na kuisaidia timu yake kushinda michuano mara mbili.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Erin Victoria Phillips alizaliwa tarehe 19 Mei 1985 katika kitongoji cha Carlton, Melbourne, kwa wazazi wake Julie na Greg Phillips.[1][2] Wakati huo baba yake alikuwa mchezaji wa kulipwa wa mpira wa miguu, akiichezea katika klabu ya Collingwood Football Club katika ligi ya Victorian Football League] (VFL; ambayo baadaye ikawa AFL). Jina lake la kati, Victoria, lilihusiana na jimbo la Victoria.

Familia yake ilihamia Adelaide, ambako Phillips alikulia pamoja na dada zake wakubwa wawili, Rachel na Amy.[3][4] Baba yake alitumia sehemu kubwa ya taaluma yake katika klabu ya Port Adelaide Football Club ya South Australian National Football League](SANFL), ambako aliwahi kuwa nahodha kwa miaka mitatu, na mwaka 2020 aliingizwa katika Australian Football Hall of Fame.[5] Phillips alisema kuwa tangu akiwa mdogo alitamani kuwa mchezaji wa AFL kama baba yake,[6] na baba yake alitambua kipaji chake cha michezo mapema.[3]

Phillips alisoma katika shule ya Seaton High School, iliyopo katika kitongoji cha magharibi mwa Adelaide kiitwacho Seaton, kipindi ambacho baba yake alikuwa akichezea Port Adelaide FC. Familia yake nzima, wakiwemo bibi, babu na shangazi zake, walihudhuria kila mechi.

Alianza kushiriki mpira wa miguu kupitia klabu ya SMOSH West Lakes Football Club (wakati huo ikiitwa St. Michael's Old Scholars and Hindmarsh Football Club) katika kikosi cha chini ya miaka 9, ambapo alikuwa msichana pekee kwenye timu. Timu yake ya chini ya miaka 11 ilitwaa ubingwa wa ligi.[1] Aidha, alipata tuzo ya mchezaji bora na mwenye nidhamu katika kikosi cha chini ya miaka 13.[7] John Cahill, mmoja wa makocha wa Port Adelaide, alimpongeza kwa uwezo wake akisema alikuwa msichana mwenye umri wa miaka 14 bora zaidi niliyewahi kumuona akicheza mpira wa miguu.[8] Mara kwa mara Phillips alipata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha Port Adelaide alipokuwa akikua.[8]

Phillips alianza kucheza mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 13.[4] Alipofikisha miaka 14, aliamua kuelekeza nguvu zake katika mpira wa kikapu kutokana na ukosefu wa fursa za wanawake kucheza mpira wa miguu kitaaluma wakati huo.[9] Katika kipindi hicho, baba yake alimjulisha kwa Rachael Sporn, mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Australia.[3] Akiwa kijana, Phillips alichezea West Adelaide Bearcats.[2] Aliiwakilisha South Australia Metro katika mashindano ya kitaifa ya chini ya miaka 16 na chini ya miaka 18, akishinda mashindano ya Norma Connolly Trophy akiwa sehemu ya kikosi cha mabingwa wa chini ya miaka 16 mwaka 1999.[10][11] Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha ubingwa cha South Australia cha chini ya miaka 20 mwaka 2004, ambako alishindatuzo ya Bob Staunton Award kama mchezaji bora wa mashindano ya wanawake.[12]


  1. 1 2 3 Hayes, Nicole; Sometimes, Alicia (2017). A Footy Girl's Guide to the Stars of 2017. Black Inc. uk. Erin Phillips. ISBN 978-1925435535.
  2. 1 2 3 Phillips, Erin (16 Januari 2018). "It's time to draw the curtain". Athlete's Voice. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Aprili 2020. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 1 2 3 "Fathers say: Before my child was a star". The Sydney Morning Herald. 1 Septemba 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1 2 "Get to Know Erin Phillips". Los Angeles Sparks. 13 Mei 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Greg Phillips". Australian Football. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Erin Phillips interview". Fox Footy AFL 360 (Fox Sports). 19 March 2019.
  7. cite podcast |title=Open Mike: Greg and Erin Phillips |url=https://player.whooshkaa.com/episode?id=136714 Ilihifadhiwa 2 Oktoba 2023 kwenye Wayback Machine. |website=Whooshkaa |publisher=Fox Footy |access-date=25 May 2020
  8. 1 2 2015 SANFL Coaches Dinner – John Cahill. South Australian National Football League. https://www.youtube.com/watch?v=iXXJmSFyUJk.
  9. McGarry, Andrew (4 Aprili 2019). "Erin Phillips's AFLW success due to mix of fitness, fierceness, strength, smarts and athleticism". Australian Broadcasting Corporation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Desemba 2019. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Erin Phillips Player Profile". SportsTG. Iliwekwa mnamo 22 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "U16 Junior Championships History". Basketball Australia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 22 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "U20 & Ivor Burge Championships History". Basketball Australia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 4 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Erin Phillips kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.