Nenda kwa yaliyomo

Kifutio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eraser)
Vifutio
Matumizi ya kifutio (raba) na kupangusa chembe zake

Kifutio au raba (kutoka Kiingereza rubber) ni kifaa kinachotumiwa kufuta alama za penseli au aina za kalamu. Kimsingi ni kipande kigumu cha mpira kinachotumiwa kufutia maandishi.

Mara nyingi kipande kidogo cha mpira kimefungwa kwenye penseli yenyewe wakati inapotengenzwa. Ilhali vipande vidogo huisha haraka au kuvunjika ni afadhali kuwa na kipande kikubwa.

Ziko aina tofauti hasa katika kiwango cha ugumu; tofauti nyingine ni uundaji kutokana na utomvu wa mpira au plastiki.

Fizikia ya kifutio - raba

[hariri | hariri chanzo]

Penseli huandika kwa kuweka grafati kwenye uso wa karatasi; vipande vya grafati hushikwa kwa nguvu ya mng'ang'aniano; ule mng'ang'aniano baina ya mpira na grafati una nguvu zaidi kuliko ule baina ya karatasi na grafati. Wakati unaburuza raba juu ya karatasi, uso wake unashikana na grafati. Hapo ni muhimu kwamba raba inaachana na vipande vya uso wake vilivyojaa grafati tayari ili sehemu mpya ya uso wake iwe tayari kupokea vipande vingine vya grafati. Hivyo matumizi ya kifutio yanaacha chembe ndogo kwenye uso wa karatasi ambazo tunaweza kuondoa kirahisi kwa kuzipangusa au kupuliza.

Kifutio cha ubao

[hariri | hariri chanzo]

Kuna pia kifutio kinachotumiwa kwenye ubao k.m. shuleni. Hicho huitwa pia dasta (ing. duster). Kwa kawaida ni kipande cha kitambaa au sifongo kinachotumiwa kuondoa alama za chaki kwenye ubao wa shule.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.