Elhanan bin Jair
Mandhari
Elhanan bin Jair (kwa Kiebrania אלחנן בן יערי) alikuwa mtu wa Bethlehemu kwenye mwaka 1000 KK.
Anatajwa na Kitabu cha Pili cha Samueli 21:19 kama muuaji wa jitu Goliathi, Mfilisti wa mji wa Gath[1][2].
Hata hivyo Kitabu cha Kwanza cha Samueli sura ya 17 kinasema kijana Daudi ndiye aliyeshindana na Goliathi akitumia kombeo na mawe akafaulu kumshinda na kumuua. Tofauti hiyo inatokana na jinsi vitabu hivyo viwili vilivyotungwa kwa kukusanya mapokeo yoyote juu ya mwanzo wa Ufalme wa Israeli bila kuyachambua[3].
Goliathi anatajwa pia katika Qur'an (2: 247–252)[4].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Halpern, Baruch (2003). David's Secret Demons: Messiah, Murderer, Traitor, King (kwa Kiingereza). Wm. B. Eerdmans Publishing. uk. 7-10. ISBN 9780802827975.
- ↑ Hays, J. Daniel (Desemba 2005). "Reconsidering the Height of Goliath" (Portable Document File). Journal of the Evangelical Theological Society. 48 (4): 701–14.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The most widely accepted explanation is that the storytellers have displaced the deed from the obscure Elhanan to the more famous character, David. David's Secret Demons, Baruch Halpern, (2004), p. 8
- ↑ Encyclopedia of Islam, G. Vajda, Djalut
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elhanan bin Jair kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |