Eisleben

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jumba la manisipaa na kanisa kuu la Eisleben
Martin Luther alifariki katika nyumba hii

Eisleben ni mji katika jimbo la Saksonia-Anhalt nchini Ujerumani. Mji huu ni mashuhuri kama mahali pa kuzaliwa kwa Martin Luther na kwa hiyo jina rasmi ni Lutherstadt Eisleben (Eisleben Mji wa Luther). Mnamo mwaka 2015 Eisleben ilikuwa na wakazi 24,198.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji huu mdogo una historia ndefu. Ilitajwa mara za kwanza katika hati ya mwaka 994 BK.

Katika karne ya 12 ulikuwa mji mkuu wa dola dogo la makabaila wa Mansfeld. Dola hili pamoja na mji wa Eisleben lilitajirika katika karne ya 13 baada ya kugunduliwa matapo ya shaba na kuanzishwa kwa migodi ya kuchimba madini haya na tasnia ya kuyeyusha shaba hapa.

Katika karne ya 18 eneo la Mansfeld ilikuwa sehemu ya milki ya Saksonia na baadaye ya Prussia. Baada ya ugawaji wa Prussia mwaka 1945 mji ulikuwa sehemu ya jimbo la Saksonia-Anhalt.

Eisleben si mji tu wa kuzaliwa kwa Luther ni pia mahali alipohubiri mara ya mwisho wa kifo na kuaga dunia. Nyumba za kuzaliwa na kufa kwake ni mahali pa makumbusho zilizopokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eisleben kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.