Nenda kwa yaliyomo

Edina Alves Batista

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edina Alves Batista (alizaliwa 10 Januari 1980) ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa chama cha soka cha Brazil. [1]

Alikuwa mwamuzi katika michezo miwili mnamo Aprili 2018 kwenye michuano ya kombe la Copa Amerika la Wanawake 2018 iliyofanyika Chile.

Aliongoza mechi kadhaa kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake 2019 pamoja na nusu fainali kati ya Uingereza na Marekani . [2]

Mwaka 2020, alikuwa mwamuzi katika mashindano ya Kandanda ya Wanawake ya Amerika Kusini 2020 yaliyofanyika nchini Argentina.

Mnamo 7 Februari 2021, alikua mwanamke wa kwanza kuchezesha katika mashindano ya FIFA ya mpira wa miguu wa wanaume, ambapo alichezesha mechi ya nafasi ya tano kati ya Ulsan Hyundai na Al-Duhail kwenye Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA la 2020 . [3] Mnamo 3 Machi 2021, alikua mwamuzi wa kwanza wa mwanamke kuchezesha mchezo wa dabi kati ya Corinthians na Palmeiras nchini Brazil. [4]

  1. "Edina Alves Batista agora é FIFA, a notícia foi oficializada pela Confederação Brasileira de Futebol" (kwa Kireno). goioere.cidadeportal.com.br. 16 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-16. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "FIFA Women's World Cup France 2019 - List of match officials" (PDF).
  3. @FIFAcom (7 Februari 2021). "History made at the #ClubWC" (Tweet) – kutoka Twitter. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "O dérbi resiste a tudo e consagra Edina Alves Batista". uol.com (kwa Portuguese). 3 Machi 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edina Alves Batista kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.